Zekaria 8:23
Zekaria 8:23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yuko pamoja nanyi.
Zekaria 8:23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hili ndilo asemalo BWANA Mwenye Nguvu Zote: “Katika siku hizo watu kumi kutoka lugha zote na mataifa, watangʼangʼania upindo wa joho la Myahudi mmoja na kusema, ‘Twende pamoja nawe kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nawe.’ ”
Zekaria 8:23 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati huo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, watu kumi kutoka mataifa ya kila lugha watamng'ang'ania Myahudi mmoja na kushika nguo yake na kumwambia, ‘Tunataka kwenda pamoja nanyi, kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.’”
Zekaria 8:23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA wa majeshi asema hivi, Siku hizo watu kumi, wa lugha zote za mataifa, wataushika upindo wa nguo yake yeye aliye Myahudi; naam, wataushika wakisema, Tutakwenda pamoja nanyi, kwa maana tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.