Zekaria 1:17-21
Zekaria 1:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha malaika huyo akaniambia nitangaze ujumbe huu mwingine: “Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: ‘Miji yangu itafurika tena fanaka. Mimi Mwenyezi-Mungu nitaufariji tena mji wa Siyoni; nitauteua mji wa Yerusalemu kuwa wangu.’” Katika maono mengine, niliona pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika aliyezungumza nami, “Pembe hizi zinamaanisha nini?” Yeye akanijibu, “Pembe hizi zinamaanisha yale mataifa ambayo yaliwatawanya watu wa Yuda, Israeli na Yerusalemu.” Kisha, Mwenyezi-Mungu akanionesha wafuachuma wanne. Nami nikauliza, “Watu hawa wanakuja kufanya nini?” Yeye akanijibu, “Watu hawa wamekuja kuyatisha na kuyaangamiza yale mataifa yenye nguvu ambayo yaliishambulia nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”
Zekaria 1:17-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Piga kelele tena, na kusema, BWANA wa majeshi asema hivi, Miji yangu itajawa na ufanisi tena; naye BWANA ataufariji Sayuni tena, atauchagua Yerusalemu tena. Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu. Kisha BWANA akanionesha wafua chuma wanne. Ndipo nikauliza, Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.
Zekaria 1:17-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Piga kelele tena, na kusema, BWANA wa majeshi asema hivi, Miji yangu kwa kufanikiwa itaenezwa huko na huko tena; naye BWANA ataufariji Sayuni tena, atauchagua Yerusalemu tena. Nami nikainua macho yangu, nikaona, na tazama, pembe nne. Nami nikamwuliza yule malaika aliyesema nami, Nini hizi? Naye akanijibu, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, na Israeli, na Yerusalemu. Kisha BWANA akanionyesha wafua chuma wanne. Ndipo nikauliza Hawa wanakuja kufanya nini? Akasema kwamba, Hizi ndizo pembe zilizowatawanya watu wa Yuda, hata ikawa hakuna mtu aliyeinua kichwa chake; lakini hawa wamekuja kuzifukuza, kuziangusha pembe za mataifa, walioinua pembe yao juu ya nchi ya Yuda, ili kuwatawanya watu wake.
Zekaria 1:17-21 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Endelea kutangaza zaidi kwamba: Hivi ndivyo asemavyo BWANA Mwenye Nguvu Zote: ‘Miji yangu itafurika tena ustawi na BWANA atamfariji tena Sayuni na kumchagua Yerusalemu.’ ” Kisha nikatazama juu, na pale mbele yangu nikaona pembe nne! Nikamuuliza yule malaika aliyekuwa akizungumza nami, “Ni nini hivi?” Akanijibu, “Hizi ni zile pembe zilizowatawanya Yuda, Israeli na Yerusalemu.” Kisha BWANA akanionyesha mafundi wanne. Nikauliza, “Hawa wanakuja kufanya nini?” Akanijibu, “Hizi ndizo pembe zilizowatawanya Yuda ili asiwepo atakayeweza kuinua kichwa chake, lakini mafundi wamekuja kuzitia hofu na kuzitupa chini hizi pembe za mataifa ambayo yaliinua pembe zao dhidi ya nchi ya Yuda na kuwatawanya watu wake.”