Ruthu 4:13-14
Ruthu 4:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo, Boazi akamchukua Ruthu akawa mke wake. Mwenyezi-Mungu alimjalia Ruthu naye akachukua mimba, akajifungua mtoto wa kiume. Ndipo wanawake wa mji huo wakamwambia Naomi, “Atukuzwe Mwenyezi-Mungu ambaye hakukuacha leo bila kuwa na jamaa aliye karibu wa kukutunza; naye awe mwenye sifa kubwa katika Israeli.
Ruthu 4:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume. Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe BWANA, asiyekuacha leo ukiwa huna jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.
Ruthu 4:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi Boazi akamtwaa Ruthu, naye akawa mke wake; naye akaingia kwake, na BWANA akamjalia kuchukua mimba, naye akazaa mtoto wa kiume. Nao wale wanawake wakamwambia Naomi, Na ahimidiwe BWANA, asiyekuacha leo hali huna wa jamaa aliye karibu; jina lake huyu na liwe kuu katika Israeli.
Ruthu 4:13-14 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Basi Boazi akamwoa Ruthu, naye akawa mke wake. Alipoingia kwake, BWANA akamjalia Ruthu, naye akapata mimba, akamzaa mtoto wa kiume. Wanawake wakamwambia Naomi: “Ahimidiwe BWANA, asiyekuacha bila kuwa na jamaa wa karibu wa kukomboa. Na awe mashuhuri katika Israeli yote!