Ruthu 3:6-11
Ruthu 3:6-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza. Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa chungu ya nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo. Na ikawa usiku wa manane yule mtu akasituka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake. Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu. Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonyesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, kama ni maskini kama ni matajiri. Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana mji wote pia wa watu wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.
Ruthu 3:6-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Basi akashuka mpaka kwenye sakafu ya kupuria, akafanya kila kitu mama mkwe wake alichomwambia kufanya. Wakati Boazi alipomaliza kula na kunywa, naye akawa amejawa na furaha, alikwenda kulala mwisho wa lundo la nafaka. Ruthu akanyemelea polepole, akafunua miguu yake, na akalala. Usiku wa manane, kitu kilimshtua Boazi, akajigeuza, akagundua yupo mwanamke amelala miguuni pake. Akauliza, “Wewe ni nani?” Akajibu, “Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kutukomboa.” Akamwambia, “Binti yangu, ubarikiwe na BWANA. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini. Sasa, binti yangu, usiogope. Nitakufanyia yote uliyoomba. Kwa maana mji wote wa watu wangu wanakujua ya kwamba wewe ni mwanamke mwenye tabia nzuri.
Ruthu 3:6-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwa hiyo, Ruthu alikwenda mahali pa kupuria, akafanya jinsi mama mkwe wake alivyomwamuru. Boazi alipomaliza kula na kunywa, akafurahi moyoni. Basi alikwenda karibu na tita la shayiri, akalala. Ruthu alikwenda polepole akafunua miguu yake na kulala hapo. Usiku wa manane, Boazi aligutuka, akageuka, akashtuka kumkuta mwanamke amelala miguuni pake. Akauliza, “Wewe ni nani?” Ruthu akajibu, “Ni mimi Ruthu, mtumishi wako. Kwa kuwa wewe u jamaa yangu wa karibu, uitande nguo yako juu ya mjakazi wako.” Boazi akasema, “Mwenyezi-Mungu na akubariki, kwa maana kwa yote unayofanya unaonesha heshima zaidi kuliko uliyoyafanya hapo awali, kwa maana hukuwatafuta vijana maskini au tajiri wakuoe. Sasa binti yangu usifadhaike, nitakufanyia lolote utakaloomba kwa kuwa kila mtu mjini humu anajua wema wako.
Ruthu 3:6-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi akashuka mpaka ugani; akafanya yote kama vile mkwewe alivyomwagiza. Ikawa huyo Boazi alipokwisha kula na kunywa, na moyo wake umekunjuka, alikwenda kulala penye mwisho wa rundo la nafaka; na huyo mwanamke akaja taratibu, akaifunua miguu yake, akajilaza papo hapo. Na ikawa usiku wa manane yule mtu akashtuka, akajigeuza; na kumbe! Yupo mwanamke amelala miguuni pake. Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu. Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri. Basi, mwanangu, usiogope; mimi nitakufanyia yote uyanenayo; kwa maana watu wote wa mjini wangu wanakujua ya kwamba u mwanamke mwema.