Ufunuo 7:3-4
Ufunuo 7:3-4 Biblia Habari Njema (BHN)
“Msiharibu nchi, wala bahari, wala miti, mpaka tutakapokwisha wapiga mhuri watumishi wa Mungu wetu katika paji la uso.” Kisha, nikasikia idadi ya hao waliopigwa mhuri: Watu 144,000 wa makabila yote ya watu wa Israeli.
Shirikisha
Soma Ufunuo 7Ufunuo 7:3-4 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.
Shirikisha
Soma Ufunuo 7Ufunuo 7:3-4 Swahili Revised Union Version (SRUV)
akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hadi tutakapokwisha kuwatia mhuri watumishi wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa mhuri katika kila kabila la Waisraeli, watu elfu mia moja na arubaini na nne.
Shirikisha
Soma Ufunuo 7