Zaburi 92:12-15
Zaburi 92:12-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Waadilifu hustawi kama mitende; hukua kama mierezi ya Lebanoni! Kama miti iliyopandwa nyumbani mwa Mwenyezi-Mungu, hustawi katika nyua za Mungu wetu; huendelea kuzaa matunda hata uzeeni; daima wamejaa utomvu na wabichi; wapate kutangaza kwamba Mwenyezi-Mungu ni mnyofu, Mwamba wangu, kwake hamna upotovu.
Zaburi 92:12-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mwenye haki atastawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Waliopandwa katika nyumba ya BWANA Watastawi katika nyua za Mungu wetu. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.
Zaburi 92:12-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mwenye haki atasitawi kama mtende, Atakua kama mwerezi wa Lebanoni. Waliopandwa katika nyumba ya BWANA Watasitawi katika nyua za Mungu wetu. Watazaa matunda hadi wakati wa uzee, Watajaa utomvu, watakuwa na ubichi. Watangaze ya kuwa BWANA ni mwenye adili, Mwamba wangu, ndani yake hamna udhalimu.
Zaburi 92:12-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wenye haki watastawi kama mtende, watakuwa kama mwerezi wa Lebanoni, waliopandwa katika nyumba ya BWANA, watastawi katika nyua za Mungu wetu. Wakati wa uzee watakuwa bado wanazaa matunda, watakuwa wabichi tena wamejaa nguvu, wakitangaza, “BWANA ni mkamilifu; yeye ni Mwamba wangu, na ndani yake hamna uovu.”