Zaburi 89:19-37
Zaburi 89:19-37 Biblia Habari Njema (BHN)
Zamani ulinena katika maono, ukawaambia watumishi wako waaminifu: “Nimempa nguvu shujaa mmoja, nimemkuza huyo niliyemteua kati ya watu. Nimempata Daudi, mtumishi wangu; nimemweka wakfu kwa mafuta yangu matakatifu. Mkono wangu wa nguvu utakuwa naye daima; mkono wangu mimi mwenyewe utamwimarisha. Maadui hawataweza kumshinda, wala waovu hawatamnyanyasa. Mimi nitawaponda wapinzani wake; nitawaangamiza wote wanaomchukia. Nitakuwa mwaminifu kwake na kumfadhili, kwa jina langu atapata ushindi mkubwa. Nitaimarisha nguvu na utawala wake, toka bahari hata mito. Yeye ataniita: ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, mwamba wa wokovu wangu.’ Nami nitamfanya kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, mkuu kuliko wafalme wote duniani. Fadhili zangu nitamwekea milele, na agano langu kwake litadumu daima. Nitaudumisha daima ukoo wake wa kifalme, na ufalme wake kama mbingu. “Lakini wazawa wake wakiiacha sheria yangu, wasipoishi kadiri ya maagizo yangu, kama wakizivunja kanuni zangu, na kuacha kutii amri zangu, hapo nitawaadhibu makosa yao; nitawapiga kwa sababu ya uovu wao. Lakini sitaacha kumfadhili Daudi, wala kuwa mwongo kuhusu uaminifu wangu. Sitavunja agano langu naye, wala kubatili neno nililotamka kwa mdomo wangu. “Nimeapa mara moja tu kwa utakatifu wangu; nami sitamwambia Daudi uongo. Ukoo wake utadumu milele; na ufalme wake kama jua. Utadumu milele kama mwezi utokezavyo angani.”
Zaburi 89:19-37 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa maono, Ukasema, Nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu. Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa. Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia. Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka. Nitaweka mkono wake juu ya bahari, Na mkono wake wa kulia juu ya mito. Yeye ataniita, Wewe ni baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wote wa dunia. Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na agano langu naye litadumu hata milele. Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu, Wakizivunja amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu, Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo. Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo. Mimi sitalivunja agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo, Wazawa wake watadumu milele, Na kiti chake cha enzi kuwa mbele yangu kama jua. Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi mwaminifu aliye mbinguni.
Zaburi 89:19-37 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Ulizungumza wakati fulani katika maono, kwa watu wako waaminifu, ukasema: “Nimeweka nguvu kwa shujaa, nimemwinua kijana miongoni mwa watu. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, na nimempaka mafuta yangu matakatifu. Kitanga changu kitamtegemeza, hakika mkono wangu utamtia nguvu. Hakuna adui atakayemtoza ushuru, hakuna mtu mwovu atakayemtesa. Nitawaponda adui zake mbele zake na kuwaangamiza watesi wake. Upendo wangu mkamilifu utakuwa pamoja naye, kwa Jina langu pembe yake itatukuzwa. Nitauweka mkono wake juu ya bahari, mkono wake wa kuume juu ya mito. Naye ataniita kwa sauti, ‘Wewe ni Baba yangu, Mungu wangu, Mwamba na Mwokozi wangu.’ Nitamteua pia awe mzaliwa wangu wa kwanza, aliyetukuka kuliko wafalme wote wa dunia. Nitadumisha upendo wangu kwake milele, na agano langu naye litakuwa imara. Nitaudumisha uzao wake milele, kiti chake cha utawala kama mbingu zinavyodumu. “Kama wanawe wataacha amri yangu na wasifuate sheria zangu, wakihalifu maagizo yangu na kutoshika amri zangu, nitaadhibu dhambi yao kwa fimbo, uovu wao kwa kuwapiga; lakini sitauondoa upendo wangu kwake, wala sitausaliti uaminifu wangu kamwe. Mimi sitavunja agano langu wala sitabadili lile ambalo midomo yangu imelitamka. Mara moja na kwa milele, nimeapa kwa utakatifu wangu, nami sitamdanganya Daudi: kwamba uzao wake utaendelea milele, na kiti chake cha enzi kitadumu mbele zangu kama jua; kitaimarishwa milele kama mwezi, shahidi mwaminifu angani.”
Zaburi 89:19-37 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ndipo ulipowaambia watakatifu wako kwa njozi, Ukasema, nimempa aliye hodari msaada; Nimemtukuza aliyechaguliwa miongoni mwa watu. Nimemwona Daudi, mtumishi wangu, Nimempaka mafuta yangu matakatifu. Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake, Na mkono wangu utamtia nguvu. Adui hatamwonea, Wala mwana wa uovu hatamtesa. Bali nitawaponda watesi wake mbele yake, Nitawapiga wanaomchukia. Uaminifu wangu na fadhili zangu atakuwa nazo, Na kwa jina langu pembe yake itatukuka. Nitaweka mkono wake juu ya bahari, Na mkono wake wa kuume juu ya mito. Yeye ataniita, Wewe baba yangu, Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu. Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza, Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia. Hata milele nitamwekea fadhili zangu, Na agano langu litafanyika amini kwake. Wazao wake nao nitawadumisha milele, Na kiti chake cha enzi kama siku za mbingu. Wanawe wakiiacha sheria yangu, Wasiende katika hukumu zangu, Wakizihalifu amri zangu, Wasiyashike maagizo yangu, Basi, nitawarudi makosa yao kwa fimbo, Na uovu wao kwa mapigo. Lakini fadhili zangu sitamwondolea yeye, Wala sitafanya uaminifu wangu kuwa uongo. Mimi sitalihalifu agano langu, Sitalibadili neno lililotoka midomoni mwangu. Neno moja nimeliapa kwa utakatifu wangu, Hakika sitamwambia Daudi uongo, Wazao wake watadumu milele, Na kiti chake kitakuwa kama jua mbele zangu. Kitathibitika milele kama mwezi; Shahidi aliye mbinguni mwaminifu.