Zaburi 86:1-7
Zaburi 86:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee BWANA, sikia na unijibu, kwa maana mimi ni maskini na mhitaji. Linda maisha yangu, kwa maana nimejiweka kwako, wewe ni Mungu wangu, mwokoe mtumishi wako anayekutumaini. Ee BWANA, nihurumie mimi, kwa maana ninakuita mchana kutwa. Mpe mtumishi wako furaha, kwa kuwa kwako wewe, Ee BWANA, ninainua nafsi yangu. Ee BWANA, wewe ni mwema na mwenye kusamehe, umejaa upendo kwa wote wakuitao. Ee BWANA, sikia maombi yangu, sikiliza kilio changu unihurumie. Katika siku ya shida yangu nitakuita, kwa maana wewe utanijibu.
Zaburi 86:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Unitegee sikio, ee Mwenyezi-Mungu, unijibu, maana mimi ni fukara na mnyonge. Uyahifadhi maisha yangu maana mimi ni mchaji wako; uniokoe mimi mtumishi wako ninayekutegemea. Wewe ni Mungu wangu; basi, unionee huruma, maana nakulilia mchana kutwa. Uifurahishe roho yangu mimi mtumishi wako, maana sala zangu nazielekeza kwako ee Bwana. Wewe, ee Bwana, u mwema na mwenye kusamehe; mwingi wa fadhili kwa wote wakuombao. Ee Mwenyezi-Mungu, uitegee sikio sala yangu; ukisikie kilio cha ombi langu. Siku za taabu nakuita, maana wewe waniitikia.
Zaburi 86:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Ee BWANA, utege sikio lako unijibu, Maana mimi ni maskini na mhitaji. Unihifadhi nafsi yangu, Maana mimi ni mcha Mungu. Wewe uliye Mungu wangu, Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini. Wewe, Bwana, unifadhili, Maana nakulilia Wewe mchana kutwa. Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana. Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao. Ee BWANA, uyasikie maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu. Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana utaniitikia.
Zaburi 86:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Ee BWANA, utege sikio lako unijibu, Maana mimi ni maskini na mhitaji Unihifadhi nafsi yangu, Maana mimi ni mcha Mungu. Wewe uliye Mungu wangu, Umwokoe mtumishi wako anayekutumaini. Wewe, Bwana, unifadhili, Maana nakulilia Wewe mchana kutwa. Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako, Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana. Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema, Umekuwa tayari kusamehe, Na mwingi wa fadhili, Kwa watu wote wakuitao. Ee BWANA, uyasikie maombi yangu; Uisikilize sauti ya dua zangu. Siku ya mateso yangu nitakuita, Kwa maana utaniitikia.