Zaburi 77:10-15
Zaburi 77:10-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kulia wake Aliye Juu. Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. Ee Mungu, njia yako iko katika utakatifu; Ni Mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa. Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu.
Zaburi 77:10-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nikasema, Ndio udhaifu wangu huo; Lakini nitaikumbuka miaka ya mkono wa kuume wake Aliye juu. Nitayakumbuka matendo ya BWANA; Naam, nitayakumbuka maajabu yako ya kale. Pia nitaitafakari kazi yako yote; Nitaziwaza habari za matendo yako. Ee Mungu, njia yako i katika utakatifu; Ni nani aliye mungu mkuu kama Mungu? Wewe ndiwe Mungu ufanyaye maajabu; Uliudhihirisha uweza wako kati ya mataifa. Kwa mkono wako umewakomboa watu wako, Wana wa Yakobo na Yusufu.
Zaburi 77:10-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo nikawaza, “Huu ndio udhaifu wangu: lakini nitakumbuka miaka ya mkono wa kuume wa Aliye Juu Sana.” Nitayakumbuka matendo ya BWANA; naam, nitaikumbuka miujiza yako ya zamani. Nitazitafakari kazi zako zote na kuyawaza matendo yako makuu. Ee Mungu, njia zako ni takatifu. Ni mungu yupi aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ndiwe Mungu utendaye miujiza, umeonyesha uwezo wako katikati ya mataifa. Kwa mkono wako wenye nguvu umewakomboa watu wako, uzao wa Yakobo na Yosefu.
Zaburi 77:10-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha nikasema, “Kinachonichoma zaidi ni kwamba, Mungu Mkuu hatendi tena kitu kwa ajili yetu!” Nitayakumbuka matendo yako, ee Mwenyezi-Mungu, naam, nitayafikiria maajabu yako ya hapo kale. Nitatafakari juu ya kazi zako, na kuwaza juu ya matendo yako makuu. Kila ufanyacho ee Mungu, ni kitakatifu. Ni mungu gani aliye mkuu kama Mungu wetu? Wewe ni Mungu unayetenda maajabu; wewe umeyaonesha mataifa uwezo wako. Kwa mkono wako wa nguvu uliwakomboa watu wako; uliwakomboa wazawa wa Yakobo na Yosefu.