Zaburi 68:19-23
Zaburi 68:19-23 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu asifiwe siku kwa siku! Yeye hutubebea mizigo yetu; yeye ndiye Mungu wa wokovu wetu. Mungu wetu ni Mungu mwenye kutuokoa; Bwana Mungu pekee ndiye aokoaye katika kifo. Mungu ataviponda vichwa vya maadui zake, naam, vichwa vya wanaoshikilia njia mbaya. Bwana alisema: “Nitawarudisha maadui kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, uoshe miguu katika damu ya maadui zako, nao mbwa wako wale shibe yao.”
Zaburi 68:19-23 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. Mungu wetu ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afululizaye kukosa. Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake.
Zaburi 68:19-23 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na ahimidiwe Bwana, Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu; Mungu ndiye wokovu wetu. Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa; Na njia za kutoka mautini zina YEHOVA Bwana. Naam, Mungu atakipasua kichwa cha adui zake, Utosi wenye nywele wa mtu afulizaye kukosa. Bwana alisema, Kutoka Bashani nitawarudisha, Nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari; Uuchovye mguu wako katika damu ya adui zako, Na ulimi wa mbwa zako upate sehemu yake.
Zaburi 68:19-23 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sifa apewe Bwana, Mungu Mwokozi wetu, ambaye siku kwa siku hutuchukulia mizigo yetu. Mungu wetu ni Mungu aokoaye, BWANA Mwenyezi hutuokoa na kifo. Hakika Mungu ataponda vichwa vya adui zake, vichwa vya hao waendao katika njia za dhambi. Bwana alisema, “Nitawarudisha kutoka Bashani; nitawarudisha kutoka vilindi vya bahari, ili uweze kuchovya miguu yako katika damu ya adui zako, huku ndimi za mbwa wako zikiwa na fungu lake.”