Zaburi 3:3-5
Zaburi 3:3-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini wewe, Ee BWANA, ni ngao pande zote; umeniwekea utukufu na kuinua kichwa changu. Ninamlilia BWANA kwa sauti kuu, naye ananijibu kutoka mlima wake mtakatifu. Ninajilaza na kupata usingizi; naamka tena, kwa maana BWANA hunitegemeza.
Zaburi 3:3-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini wewe ee Mwenyezi-Mungu u ngao yangu kila upande; kwako napata fahari na ushindi wangu. Nakulilia kwa sauti, ee Mungu, nawe wanisikiliza kutoka mlima wako mtakatifu. Nalala na kupata usingizi, naamka tena maana wewe ee Mwenyezi-Mungu wanitegemeza.
Zaburi 3:3-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nilijilaza na kulala usingizi, kisha ninaamka tena, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.
Zaburi 3:3-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na Wewe, BWANA, U ngao yangu pande zote, Utukufu wangu na mwinua kichwa changu. Kwa sauti yangu namwita BWANA Naye aniitikia toka mlima wake mtakatifu. Nalijilaza nikalala usingizi, nikaamka, Kwa kuwa BWANA ananitegemeza.