Zaburi 24:1-10
Zaburi 24:1-10 Biblia Habari Njema (BHN)
Dunia na vyote vilivyomo ni vyake Mwenyezi-Mungu; ulimwengu na wote waishio humo ni mali yake. Maana yeye aliweka misingi ya dunia juu ya bahari; aliisimika imara juu ya mito ya maji. Nani atakayepanda mlima wa Mwenyezi-Mungu? Nani atakayekaa katika hekalu lake takatifu? Ni mtu wa matendo mema na moyo safi, asiyeuelekeza moyo wake katika upuuzi, wala kuapa kwa uongo. Mtu huyo atapokea baraka kwa Mwenyezi-Mungu, na haki yake kwa Mungu mwokozi wake. Ndio hali ya kizazi cha watu wamtafutao yeye; naam, watu wamtafutao Mungu wa Yakobo. Fungukeni enyi milango; fungukeni enyi milango ya kale, ili Mfalme mtukufu aingie. Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, mwenye nguvu na uwezo; Mwenyezi-Mungu, mwenye uwezo vitani. Fungukeni enyi malango, fungukeni enyi milango ya kale, ili Mfalme mtukufu aingie. Ni nani huyo Mfalme mtukufu? Ni Mwenyezi-Mungu, wa majeshi, yeye ndiye Mfalme mtukufu.
Zaburi 24:1-10 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nchi na vyote vilivyomo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiweka nafsi yake katika uongo, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari, BWANA hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Zaburi 24:1-10 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya BWANA, Dunia na wote wakaao ndani yake. Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari, Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. Ni nani atakayepanda katika mlima wa BWANA? Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake? Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili, Wala hakuapa kwa hila. Atapokea baraka kwa BWANA, Na haki kwa Mungu wa wokovu wake. Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao, Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Inukeni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani Mfalme wa utukufu? BWANA mwenye nguvu, hodari, BWANA hodari wa vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, Naam, viinueni, enyi malango ya milele, Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? BWANA wa majeshi, Yeye ndiye Mfalme wa utukufu.
Zaburi 24:1-10 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Dunia ni mali ya BWANA, na vyote vilivyomo ndani yake, ulimwengu, na wote waishio ndani yake, maana aliiwekea misingi yake baharini na kuifanya imara juu ya maji. Nani awezaye kuupanda mlima wa BWANA? Ni nani awezaye kusimama patakatifu pake? Ni yule mwenye mikono safi na moyo mweupe, yule ambaye hakuinulia sanamu nafsi yake au kuapa kwa kitu cha uongo. Huyo atapokea baraka kutoka kwa BWANA, na hukumu ya haki kutoka kwa Mungu Mwokozi wake. Hiki ndicho kizazi cha wale wamtafutao, wale wautafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, inukeni enyi milango ya kale, ili mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani huyu Mfalme wa utukufu? Ni BWANA aliye na nguvu na uweza, ni BWANA aliye hodari katika vita. Inueni vichwa vyenu, enyi malango, viinueni juu enyi milango ya kale, ili Mfalme wa utukufu apate kuingia. Ni nani yeye, huyu Mfalme wa utukufu? Ni BWANA Mwenye Nguvu Zote; yeye ndiye Mfalme wa utukufu.