Zaburi 19:7-11
Zaburi 19:7-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia hekima mtu asiye nayo. Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru. Kicho cha BWANA ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za BWANA ni kweli, Zina haki kabisa. Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali. Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu kuu.
Zaburi 19:7-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Sheria ya BWANA ni kamilifu, Huiburudisha nafsi. Ushuhuda wa BWANA ni amini, Humtia mjinga hekima. Maagizo ya BWANA ni ya adili, Huufurahisha moyo. Amri ya BWANA ni safi, Huyatia macho nuru. Kicho cha BWANA ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za BWANA ni kweli, Zina haki kabisa. Ni za kutamanika kuliko dhahabu, Kuliko wingi wa dhahabu safi. Nazo ni tamu kuliko asali, Kuliko sega la asali. Tena mtumishi wako huonywa kwazo, Katika kuzishika kuna thawabu nyingi.
Zaburi 19:7-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Sheria ya Mwenyezi-Mungu ni kamilifu, humpa mtu uhai mpya; masharti ya Mwenyezi-Mungu ni thabiti, huwapa hekima wasio na makuu. Kanuni za Mwenyezi-Mungu ni sawa, huufurahisha moyo; amri ya Mwenyezi-Mungu ni safi, humwelimisha mtu. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni jambo jema, na la kudumu milele; maagizo ya Mwenyezi-Mungu ni sawa, yote ni ya haki kabisa. Yatamanika kuliko dhahabu; kuliko dhahabu safi kabisa. Ni matamu kuliko asali; kuliko asali safi kabisa. Yanifunza mimi mtumishi wako; kuyafuata kwaniletea tuzo kubwa.
Zaburi 19:7-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sheria ya BWANA ni kamilifu, ikihuisha nafsi. Shuhuda za BWANA ni za kuaminika, zikimpa mjinga hekima. Maagizo ya BWANA ni kamili, nayo hufurahisha moyo. Amri za BWANA huangaza, zatia nuru machoni. Kumcha BWANA ni utakatifu, nako kwadumu milele. Amri za BWANA ni za hakika, nazo zina haki. Ni za thamani kuliko dhahabu, kuliko dhahabu iliyo safi sana, ni tamu kuliko asali, kuliko asali kutoka kwenye sega. Kwa hizo mtumishi wako anaonywa, katika kuzishika kuna thawabu kubwa.