Zaburi 18:16-30
Zaburi 18:16-30 Biblia Habari Njema (BHN)
Mungu alinyosha mkono kutoka juu akanichukua, kutoka katika maji mengi alininyanyua. Aliniokoa kutoka kwa maadui zangu wenye nguvu nyingi, aliniokoa kutoka kwa hao walionichukia, maana walikuwa na nguvu kunishinda. Walinivamia nilipokuwa taabuni, lakini Mwenyezi-Mungu alikuwa kinga yangu. Alinileta, akaniweka mahali pa usalama; alinisalimisha, kwani alipendezwa nami. Mwenyezi-Mungu alinipa tuzo kadiri ya uadilifu wangu; alinituza kwa vile mikono yangu haina hatia. Maana nimefuata njia za Mwenyezi-Mungu, wala sikujitenga na Mungu wangu kwa uovu. Nimeshika maagizo yake yote, sikuacha kufuata masharti yake. Mbele yake sikuwa na hatia; nimejikinga nisiwe na hatia. Mwenyezi-Mungu amenituza kadiri ya uadilifu wangu; yeye ajua kwamba mikono yangu haina hatia. Wewe ni mwaminifu kwa walio waaminifu; mwema kwa wale walio wema. Wewe ni mkamilifu kwa walio wakamilifu; lakini mkatili kwa watu walio waovu. Wewe wawaokoa walio wanyenyekevu, lakini wenye majivuno huwaporomosha. Wewe ee Mwenyezi-Mungu, waniangazia; walifukuza giza langu, ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu. Kwa msaada wako nakishambulia kikosi; wewe wanipa nguvu ya kuruka ukuta. Huyu Mungu matendo yake hayana dosari! Ahadi ya Mwenyezi-Mungu ni ya kuaminika; yeye ni ngao kwa wote wanaomkimbilia usalama.
Zaburi 18:16-30 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Alinishukia kutoka juu, akanichukua, Na kunitoa katika maji mengi. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi. Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi Mungu wangu. Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu, Wala amri zake sikubandukana nazo. Nami nilikuwa mkamilifu mbele zake, Nikajilinda na uovu wangu. Ndipo BWANA akanilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake. Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionesha kuwa mkamilifu; Kwake ajitakasaye utajionesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionesha kuwa mkaidi. Maana Wewe wawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili. Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu; BWANA Mungu wangu aniangazia giza langu. Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta. Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya BWANA imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.
Zaburi 18:16-30 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Alipeleka kutoka juu akanishika, Na kunitoa katika maji mengi. Akaniokoa na adui yangu mwenye nguvu, Na wale walionichukia, Maana walikuwa na nguvu kuliko mimi. Walinikabili siku ya msiba wangu, Lakini BWANA alikuwa tegemeo langu. Akanitoa akanipeleka panapo nafasi, Aliniponya kwa kuwa alipendezwa nami. BWANA alinitendea sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu akanilipa. Maana nimezishika njia za BWANA, Wala sikumwasi Mungu wangu. Hukumu zake zote zilikuwa mbele yangu, Wala amri zake sikujiepusha nazo. Nami nalikuwa mkamilifu mbele zake, Nikajilinda na uovu wangu. Mradi BWANA amenilipa sawasawa na haki yangu, Sawasawa na usafi wa mikono yangu mbele zake. Kwa mtu mwenye fadhili utakuwa mwenye fadhili; Kwa mkamilifu utajionyesha kuwa mkamilifu; Kwake ajitakasaye utajionyesha kuwa mtakatifu; Na kwa mpotovu utajionyesha kuwa mkaidi. Maana Wewe utawaokoa watu wanaoonewa, Na macho ya kiburi utayadhili. Kwa kuwa Wewe unaiwasha taa yangu; BWANA Mungu wangu aniangazia giza langu. Maana kwa msaada wako nafuatia jeshi, Kwa msaada wa Mungu wangu naruka ukuta. Mungu, njia yake ni kamilifu, Ahadi ya BWANA imehakikishwa, Yeye ndiye ngao yao. Wote wanaomkimbilia.
Zaburi 18:16-30 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika; alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu. Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi, kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi. Walinikabili siku ya msiba wangu, lakini BWANA alikuwa msaada wangu. Alinileta nje mahali penye nafasi tele, akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami. BWANA alinitendea sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa. Kwa maana nimezishika njia za BWANA; sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu. Sheria zake zote zi mbele yangu, wala sijayaacha maagizo yake. Nimekuwa sina hatia mbele zake, nami nimejilinda nisitende dhambi. BWANA amenilipa sawasawa na uadilifu wangu; sawasawa na usafi wa mikono yangu machoni pake. Kwa yeye aliye mwaminifu, unajionyesha kuwa mwaminifu, kwa asiye na hatia, unajionyesha kutokuwa na hatia. Kwa aliye mtakatifu, unajionyesha kuwa mtakatifu, lakini kwa aliyepotoka, unajionyesha kuwa mkaidi. Wewe huwaokoa wanyenyekevu, lakini huwashusha wenye kiburi. Wewe, Ee BWANA, unaifanya taa yangu iendelee kuwaka; Mungu wangu hulifanya giza langu kuwa mwanga. Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi, nikiwa pamoja na Mungu wangu nitaweza kuruka ukuta. Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu, neno la BWANA halina dosari. Yeye ni ngao kwa wote wanaokimbilia kwake.