Zaburi 16:1-6
Zaburi 16:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Unilinde ee Mungu; maana kwako nakimbilia usalama. Namwambia Mungu: “Wewe u Bwana wangu; sina jema lolote ila wewe.” Ni bora sana hao watakatifu walioko nchini, kukaa nao ndiyo furaha yangu. Lakini wanaoabudu miungu mingine, watapata mateso mengi. Tambiko ya damu sitaitolea kamwe, na majina ya miungu hiyo sitayataja. Wewe ee Mwenyezi-Mungu ndiwe riziki yangu kuu, majaliwa yangu yamo mikononi mwako. Umenipimia sehemu nzuri sana; naam, urithi wangu ni wa kupendeza.
Zaburi 16:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe. Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu; Sina wema ila utokao kwako. Nao watakatifu waliopo duniani, ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. Huzuni zao zitaongezeka Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu. BWANA ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unayaamua maisha yangu. Mipaka yangu imeangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.
Zaburi 16:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mungu, unihifadhi mimi, Kwa maana nakukimbilia Wewe. Nimemwambia BWANA, Ndiwe BWANA wangu; Sina wema ila utokao kwako. Watakatifu waliopo duniani ndio Walio bora, Hao ndio niliopendezwa nao. Huzuni zao zitaongezeka Wambadilio Mungu kwa mwingine; Sitazimimina sadaka zao za damu, Wala kuyataja majina yao midomoni mwangu. BWANA ndiye fungu la posho langu, Na la kikombe changu; Wewe unaishika kura yangu. Kamba zangu zimeniangukia mahali pema, Naam, nimepata urithi mzuri.
Zaburi 16:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ee Mungu, uniweke salama, kwa maana kwako nimekimbilia. Nilimwambia BWANA, “Wewe ndiwe Bwana wangu; pasipo wewe sina jambo jema.” Kwa habari ya watakatifu walioko duniani, ndio walio wa fahari ambao ninapendezwa nao. Huzuni itaongezeka kwa wale wanaokimbilia miungu mingine. Sitazimimina sadaka zao za damu au kutaja majina yao midomoni mwangu. BWANA umeniwekea fungu langu na kikombe changu; umeyafanya mambo yangu yote yawe salama. Alama za mipaka zimeniangukia mahali pazuri, hakika nimepata urithi mzuri.