Zaburi 15:1-5
Zaburi 15:1-5 Biblia Habari Njema (BHN)
Nani ee Mwenyezi-Mungu atakayekaa hemani mwako? Nani atakayeishi juu ya mlima wako mtakatifu? Ni mtu aishiye bila lawama, atendaye daima yaliyo mema, asemaye ukweli kutoka moyoni; ni mtu asiyesengenya watu, asiyemtendea uovu rafiki yake, wala kumfitini jirani yake; ni mtu anayewadharau wafisadi, lakini huwaheshimu wamchao Mwenyezi-Mungu; ni mtu asiyegeuza kiapo chake hata kikimtia hasara; asiyekopesha fedha yake kwa riba, wala kupokea rushwa kumdhulumu asiye na hatia. Mtu atendaye hayo, kamwe hatatikisika.
Zaburi 15:1-5 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayeishi Katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala kumtenda mwenziwe mabaya, Wala kumsengenya jirani yake. Anayedharau waovu Machoni pake, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Aliyeapa ingawa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake. Asiyetoa fedha yake apate kula riba, Asiyepokea rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
Zaburi 15:1-5 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA, ni nani atakayekaa Katika hema yako? Ni nani atakayefanya maskani yake Katika kilima chako kitakatifu? Ni mtu aendaye kwa ukamilifu, Na kutenda haki. Asemaye kweli kwa moyo wake, Asiyesingizia kwa ulimi wake. Wala hakumtenda mwenziwe mabaya, Wala hakumsengenya jirani yake. Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa, Bali huwaheshimu wamchao BWANA Ingawa ameapa kwa hasara yake, Hayabadili maneno yake. Hakutoa fedha yake apate kula riba, Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia. Mtu atendaye mambo hayo Hataondoshwa milele.
Zaburi 15:1-5 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA, ni nani awezaye kukaa katika Hekalu lako? Nani awezaye kuishi katika mlima wako mtakatifu? Ni yule aendaye pasipo mawaa, atendaye yaliyo haki, asemaye kweli toka moyoni mwake, na hana masingizio ulimini mwake, asiyemtenda jirani yake vibaya, na asiyemsingizia mwenzake, ambaye humdharau mtu mbaya, lakini huwaheshimu wale wamwogopao BWANA, yule atunzaye kiapo chake hata kama anaumia. Yeye akopeshaye fedha yake bila riba, na hapokei rushwa dhidi ya mtu asiye na hatia.