Zaburi 148:13-14
Zaburi 148:13-14 Biblia Habari Njema (BHN)
Nyote lisifuni jina la Mwenyezi-Mungu, maana jina lake peke yake latukuka; utukufu wake wapita dunia na mbingu. Amewapa watu wake nguvu; heshima kwa watu wote waaminifu, watu wa Israeli wapenzi wake. Msifuni Mwenyezi-Mungu!
Zaburi 148:13-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu. Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.
Zaburi 148:13-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na walisifu jina la BWANA, Maana jina lake peke yake limetukuka; Adhama yake i juu ya nchi na mbingu. Naye amewainulia watu wake pembe, Sifa za watauwa wake wote; Wana wa Israeli, watu walio karibu naye. Haleluya.
Zaburi 148:13-14 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Wote na walisifu jina la Mwenyezi Mungu, kwa maana jina lake pekee limetukuka, utukufu wake uko juu ya nchi na mbingu. Amewainulia watu wake pembe, sifa ya watakatifu wake wote, ya Israeli, watu walio karibu na moyo wake.