Zaburi 144:1-3
Zaburi 144:1-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Atukuzwe Mwenyezi-Mungu, mwamba wangu, anayeipa mikono yangu mazoezi ya vita, na kuvifunza vidole vyangu kupigana. Yeye ni rafiki yangu amini na ngome yangu, kinga yangu na mkombozi wangu; yeye ni ngao yangu, kwake napata usalama; huyashinda mataifa na kuyaweka chini yangu. Ee Mwenyezi-Mungu, mtu ni nini hata umjali? Mwanadamu ni nini hata umfikirie?
Zaburi 144:1-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Aifundishaye mikono yangu vita, Na vidole vyangu kupigana. Mwamba wangu na ngome yangu, Nguzo yangu na mwokozi wangu Ngao yangu ninayemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu. Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjali? Na binadamu hata umwangalie?
Zaburi 144:1-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na ahimidiwe BWANA, mwamba wangu, Anifundishaye mikono yangu vita, Vidole vyangu kupigana. Mhisani wangu na boma langu, Ngome yangu na mwokozi wangu, Ngao yangu niliyemkimbilia, Huwatiisha watu wangu chini yangu. Ee BWANA, mtu ni kitu gani hata umjue? Na binadamu hata umwangalie?
Zaburi 144:1-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Sifa ni kwa BWANA Mwamba wangu, aifundishaye mikono yangu vita, na vidole vyangu kupigana. Yeye ni Mungu wangu wa upendo na boma langu, ngome yangu na mwokozi wangu, ngao yangu ninayemkimbilia, ambaye huwatiisha mataifa chini yangu. Ee BWANA, mwanadamu ni nini hata umjali, Binadamu ni nini hata umfikirie?