Zaburi 136:1-26
Zaburi 136:1-26 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mshukuruni BWANA, kwa kuwa ni mwema. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa miungu. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana: Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye pekee atendaye maajabu makuu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye kwa ufahamu wake aliziumba mbingu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliitandaza dunia juu ya maji, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliumba mianga mikubwa, Fadhili zake zadumu milele. Jua litawale mchana, Fadhili zake zadumu milele. Mwezi na nyota vitawale usiku, Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye aliyemuua mzaliwa wa kwanza wa Misri, Fadhili zake zadumu milele. Na kuwatoa Israeli katikati yao, Fadhili zake zadumu milele. Kwa mkono wenye nguvu ulionyooshwa, Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. Na kuwapitisha Israeli katikati yake, Fadhili zake zadumu milele. Lakini alimfagia Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu, Fadhili zake zadumu milele. Kwake yeye aliyewaongoza watu wake katika jangwa, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye aliwapiga wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. Naye aliwaua wafalme wenye nguvu, Fadhili zake zadumu milele. Sihoni mfalme wa Waamori, Fadhili zake zadumu milele. Ogu mfalme wa Bashani, Fadhili zake zadumu milele. Akatoa nchi yao kuwa urithi, Fadhili zake zadumu milele. Urithi kwa Israeli mtumishi wake, Fadhili zake zadumu milele. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu, Fadhili zake zadumu milele. Alituweka huru toka adui zetu, Fadhili zake zadumu milele. Ambaye humpa chakula kila kiumbe. Fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa mbinguni, Fadhili zake zadumu milele.
Zaburi 136:1-26 Biblia Habari Njema (BHN)
Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa kuwa ni mwema; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye peke yake atendaye makuu ya ajabu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeziumba mbingu kwa hekima; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeitengeneza nchi juu ya vilindi vya maji; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeumba jua, mwezi na nyota; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Jua liutawale mchana; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mwezi na nyota vitawale usiku; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyewaua wazaliwa wa kwanza wa Misri; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Akawaondoa watu wa Israeli kutoka huko; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Kwa mkono wake wenye nguvu na enzi; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyeigawa Bahari ya Shamu sehemu mbili; kwa maana fadhili zake zadumu milele, akawapitisha watu wa Israeli humo; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Lakini akawazamisha humo Farao na jeshi lake; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyewaongoza watu wake jangwani; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyewapiga wafalme wenye nguvu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Akawaua wafalme maarufu; kwa maana fadhili zake zadumu milele; akamuua Sihoni, mfalme wa Waamori, kwa maana fadhili zake zadumu milele; na Ogu, mfalme wa Bashani; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Akachukua nchi zao akawapa watu wake; kwa maana fadhili zake zadumu milele; ziwe riziki ya Israeli, mtumishi wake; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye aliyetukumbuka wakati wa unyonge wetu; kwa maana fadhili zake zadumu milele; akatuokoa kutoka maadui zetu; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Ndiye akipaye kila kiumbe chenye uhai chakula; kwa maana fadhili zake zadumu milele. Mshukuruni Mungu wa mbinguni; kwa maana fadhili zake zadumu milele!
Zaburi 136:1-26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeumba mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeumba mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wao wa kwanza; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye akipaye kila kiumbe chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.
Zaburi 136:1-26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa miungu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Bwana wa mabwana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye peke yake afanya maajabu makuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyefanya mbingu kwa fahamu zake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeitandaza nchi juu ya maji; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyefanya mianga mikubwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Jua litawale mchana; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mwezi na nyota zitawale usiku; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga Wamisri kwa kuwaua wazaliwa wa kwanza wao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawatoa Waisraeli katikati yao; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kwa mkono hodari na mkono ulionyoshwa; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyeigawa Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawavusha Israeli katikati yake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akamwangusha Farao na jeshi lake katika Bahari ya Shamu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewaongoza watu wake jangwani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Yeye aliyewapiga wafalme wakuu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akawaua wafalme mashuhuri; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Sihoni, mfalme wa Waamori; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Na Ogu, mfalme wa Bashani; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akaitoa nchi yao iwe urithi; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Urithi wa Israeli mtumishi wake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Aliyetukumbuka katika unyonge wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Akatuokoa na watesi wetu; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Kila chenye mwili akipa chakula chake; Kwa maana fadhili zake ni za milele. Mshukuruni Mungu wa mbingu; Kwa maana fadhili zake ni za milele.