Zaburi 126:1-6
Zaburi 126:1-6 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu alipoturekebisha na kuturudisha Siyoni, tulikuwa kama watu wanaoota ndoto! Hapo tuliangua kicheko; tulishangilia kwa furaha. Nao watu wa mataifa mengine walisema: “Mwenyezi-Mungu amewatendea mambo makubwa!” Kweli Mwenyezi-Mungu alitutendea mambo makubwa, tulifurahi kwelikweli! Ee Mwenyezi-Mungu, urekebishe tena hali yetu, kama mvua inavyotiririsha maji katika mabonde makavu. Wanaopanda kwa machozi, watavuna kwa shangwe. Wanaokwenda kupanda mbegu wakilia, watarudi kwa furaha wakichukua mavuno.
Zaburi 126:1-6 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA alipowarejesha mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu. BWANA alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.
Zaburi 126:1-6 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA alipowarejeza mateka wa Sayuni, Tulikuwa kama waotao ndoto. Ndipo kinywa chetu kilipojaa kicheko, Na ulimi wetu kelele za furaha. Ndipo waliposema katika mataifa, BWANA amewatendea mambo makuu. BWANA alitutendea mambo makuu, Tulikuwa tukifurahi. Ee BWANA, uwarejeze watu wetu waliofungwa, Kama vijito vya Kusini. Wapandao kwa machozi Watavuna kwa kelele za furaha. Ingawa mtu anakwenda zake akilia, Azichukuapo mbegu za kupanda. Hakika atarudi kwa kelele za furaha, Aichukuapo miganda yake.
Zaburi 126:1-6 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
BWANA alipowarejeza mateka Sayuni, tulikuwa kama watu walioota ndoto. Vinywa vyetu vilijaa kicheko, ndimi zetu zilijaa nyimbo za shangwe. Ndipo iliposemwa miongoni mwa mataifa, “BWANA amewatendea mambo makuu.” BWANA ametutendea mambo makuu, nasi tumejaa furaha. Ee BWANA, turejeshee watu wetu waliotekwa, kama vijito katika Negebu. Wapandao kwa machozi watavuna kwa nyimbo za shangwe. Yeye azichukuaye mbegu zake kwenda kupanda, huku akilia, atarudi kwa nyimbo za shangwe, akichukua miganda ya mavuno yake.