Zaburi 119:25-32
Zaburi 119:25-32 Biblia Habari Njema (BHN)
Nagaagaa chini mavumbini; unipe tena uhai kama ulivyoahidi. Nimeungama niliyotenda, nawe ukanijibu; unifundishe masharti yako. Unifundishe namna ya kushika kanuni zako, nami nitayatafakari matendo yako ya ajabu. Niko hoi kwa uchungu; unirudishie nguvu kama ulivyoahidi. Uniepushe na njia za upotovu; unifundishe kwa wema sheria yako. Nimechagua njia ya uaminifu; nimezingatia maagizo yako. Nazingatia maamuzi yako, ee Mwenyezi-Mungu; usikubali niaibishwe! Nitafuata maelekezo ya amri zako, maana unanipa maarifa zaidi.
Zaburi 119:25-32 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nafsi yangu imegandamia mavumbini, Unihuishe sawasawa na neno lako. Nilizisimulia njia zangu ukanijibu, Unifundishe amri zako. Unifahamishe njia ya maagizo yako, Nami nitayatafakari maajabu yako. Nafsi yangu imeyeyuka kwa huzuni, Unitie nguvu sawasawa na neno lako. Uniondolee njia ya uongo, Unineemeshe kwa sheria yako. Nimeichagua njia ya uaminifu, Na kuziweka hukumu zako mbele yangu. Nimeambatana na shuhuda zako, Ee BWANA, usiniaibishe. Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponipanulia ufahamu wangu.
Zaburi 119:25-32 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nafsi yangu imeambatana na mavumbi, Unihuishe sawasawa na neno lako. Nalizisimulia njia zangu ukanijibu, Unifundishe amri zako. Unifahamishe njia ya mausia yako, Nami nitayatafakari maajabu yako. Nafsi yangu imeyeyuka kwa uzito, Unitie nguvu sawasawa na neno lako. Uniondolee njia ya uongo, Unineemeshe kwa sheria yako. Nimeichagua njia ya uaminifu, Na kuziweka hukumu zako mbele yangu. Nimeambatana na shuhuda zako, Ee BWANA, usiniaibishe. Nitakwenda mbio katika njia ya maagizo yako, Utakaponikunjua moyo wangu.
Zaburi 119:25-32 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nimelazwa chini mavumbini, yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako. Nilikueleza njia zangu ukanijibu, nifundishe sheria zako. Nijulishe mafundisho ya mausia yako, nami nitatafakari maajabu yako. Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni, uniimarishe sawasawa na neno lako. Niepushe na njia za udanganyifu, kwa neema unifundishe sheria zako. Nimechagua njia ya kweli, nimekaza moyo wangu katika sheria zako. Nimengʼangʼania sheria zako, Ee BWANA, usiniache niaibishwe. Nakimbilia katika njia ya maagizo yako, kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.