Zaburi 119:11-15
Zaburi 119:11-15 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Kwa midomo yangu nimezisimulia Hukumu zote za kinywa chako. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni mali mengi. Nitayatafakari maagizo yako, Na kuziangalia njia zako.
Zaburi 119:11-15 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Ee BWANA, umehimidiwa, Unifundishe amri zako. Kwa midomo yangu nimezisimulia Hukumu zote za kinywa chako. Nimeifurahia njia ya shuhuda zako Kana kwamba ni mali mengi. Nitayatafakari mausia yako, Nami nitaziangalia njia zako.
Zaburi 119:11-15 Biblia Habari Njema (BHN)
Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea. Utukuzwe, ee Mwenyezi-Mungu! Unifundishe masharti yako. Nitayarudia kwa sauti maagizo yako yote uliyotoa. Nafurahi kufuata maamuzi yako, kuliko kuwa na utajiri mwingi. Nazitafakari kanuni zako, na kuzizingatia njia zako.
Zaburi 119:11-15 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi. Sifa ni zako, Ee BWANA, nifundishe maagizo yako. Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote zinazotoka katika kinywa chako. Ninafurahia kufuata sheria zako kama mtu afurahiaye mali nyingi. Ninatafakari maagizo yako na kuziangalia njia zako.