Zaburi 119:1-11
Zaburi 119:1-11 Biblia Habari Njema (BHN)
Heri watu wanaoishi bila kosa, wanaozingatia sheria ya Mwenyezi-Mungu. Heri wanaozingatia matakwa yake, wanaomtafuta kwa moyo wao wote, watu wasiotenda uovu kamwe, bali daima hufuata njia zake. Ee Mungu, umetupatia kanuni zako ili tuzishike kwa uaminifu. Laiti mwenendo wangu ungeimarika, kwa kuyafuata masharti yako! Nikizingatia amri zako zote, hapo kweli sitaaibishwa. Nitakusifu kwa moyo mnyofu, nikijifunza maagizo yako maadilifu. Nitayafuata masharti yako; usiniache hata kidogo. Kijana atatunzaje maisha yake kuwa safi? Kwa kuyaongoza kadiri ya neno lako. Najitahidi kukutii kwa moyo wote; usiniache nikiuke amri zako. Nimeshika neno lako moyoni mwangu, nisije nikakukosea.
Zaburi 119:1-11 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA. Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote. Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake. Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana. Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako. Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa. Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Zaburi 119:1-11 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Heri walio kamili njia zao, Waendao katika sheria ya BWANA. Heri wazitiio shuhuda zake, Wamtafutao kwa moyo wote. Naam, hawakutenda ubatili, Wamekwenda katika njia zake. Wewe umetuamuru mausia yako, Ili sisi tuyatii sana. Ningependa njia zangu ziwe thabiti, Nizitii amri zako. Ndipo mimi sitaaibika, Nikiyaangalia maagizo yako yote. Nitakushukuru kwa unyofu wa moyo, Nikiisha kujifunza hukumu za haki yako Nitazitii amri zako, Usiniache kabisa Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, Usiniache nipotee mbali na maagizo yako. Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi.
Zaburi 119:1-11 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Heri wale walio waadilifu katika njia zao, wanaoenenda katika sheria ya BWANA. Heri wale wanaozishika shuhuda zake, wamtafutao kwa moyo wao wote. Wasiofanya lolote lililo baya, wanaoenenda katika njia zake. Umetoa maagizo yako ili tuyatii kwa ukamilifu. Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara katika kuyatii maagizo yako! Hivyo mimi sitaaibishwa ninapozingatia amri zako zote. Nitakusifu kwa moyo mnyofu ninapojifunza sheria zako za haki. Nitayatii maagizo yako; usiniache kabisa. BWANA Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani? Ni kwa kutii, akilifuata neno lako. Ninakutafuta kwa moyo wangu wote, usiniache niende mbali na amri zako. Nimelificha neno lako moyoni mwangu ili nisikutende dhambi.