Zaburi 11:1-7
Zaburi 11:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Kwake Mwenyezi-Mungu nakimbilia usalama; mnawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege, mpaka milimani, maana waovu wanavuta pinde; wameweka mishale tayari juu ya uta, wawapige mshale watu wema gizani! Kama misingi ikiharibiwa, mtu mwadilifu atafanya nini?” Mwenyezi-Mungu yumo katika hekalu lake takatifu; kiti cha enzi cha Mwenyezi-Mungu kiko mbinguni. Kwa macho yake huwachungulia wanadamu, na kujua kila kitu wanachofanya. Mwenyezi-Mungu huwapima waadilifu na waovu; huwachukia kabisa watu wakatili. Atawanyeshea waovu makaa ya moto na madini ya kiberiti; upepo wa hari utakuwa ndio adhabu yao. Mwenyezi-Mungu ni mwadilifu na apenda uadilifu; watu wanyofu watakaa pamoja naye.
Zaburi 11:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu? Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo. Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini? BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawapima wanadamu. BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu. Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao. Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watauona uso wake.
Zaburi 11:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ndiye niliyemkimbilia. Mbona mnaiambia nafsi yangu, Kimbia kama ndege mlimani kwenu? Maana, tazama, wasio haki wanaupinda uta, Wanaitia mishale yao katika upote, Ili kuwapiga gizani wanyofu wa moyo. Kama misingi ikiharibika, Mwenye haki atafanya nini? BWANA yu katika hekalu lake takatifu. BWANA ambaye kiti chake kiko mbinguni, Macho yake yanaangalia; Kope zake zinawajaribu wanadamu. BWANA humjaribu mwenye haki; Bali nafsi yake humchukia asiye haki, Na mwenye kupenda udhalimu. Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa hari, Na viwe fungu la kikombe chao. Kwa kuwa BWANA ndiye mwenye haki, Apenda matendo ya haki, Wanyofu wa moyo watamwona uso wake.
Zaburi 11:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kwa BWANA ninakimbilia, unawezaje basi kuniambia: “Ruka kama ndege kwenye mlima wako. Hebu tazama, waovu wanapinda pinde zao, huweka mishale kwenye uzi wake, wakiwa gizani ili kuwapiga wale wanyofu wa moyo. Wakati misingi imeharibiwa, mwenye haki anaweza kufanya nini?” BWANA yuko ndani ya Hekalu lake takatifu; BWANA yuko kwenye kiti chake cha enzi mbinguni. Huwaangalia wana wa watu, macho yake yanawajaribu. BWANA huwajaribu wenye haki, lakini waovu na wanaopenda jeuri, nafsi yake huwachukia. Atawanyeshea waovu makaa ya moto mkali na kiberiti kinachowaka, upepo wenye joto kali ndio fungu lao. Kwa kuwa BWANA ni mwenye haki, yeye hupenda haki. Wanyofu watauona uso wake.