Zaburi 107:19-22
Zaburi 107:19-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Ndipo katika taabu yao wakamlilia Mwenyezi-Mungu, naye akawaokoa katika mateso yao. Kwa neno lake aliwaponya, akawaokoa wasiangamie. Mshukuruni Mwenyezi-Mungu kwa fadhili zake; kwa sababu ya maajabu aliyowatendea binadamu. Wamtolee tambiko za shukrani; wasimulie matendo yake kwa nyimbo za shangwe.
Zaburi 107:19-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya kutoka kwa shida zao. Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba.
Zaburi 107:19-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakamlilia BWANA katika dhiki zao, Akawaponya na shida zao. Hulituma neno lake, huwaponya, Huwatoa katika maangamizo yao. Na wamshukuru BWANA kwa fadhili zake, Na maajabu yake kwa wanadamu. Na wamtolee dhabihu za kushukuru, Na kuyasimulia matendo yake kwa kuimba.
Zaburi 107:19-22 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Ndipo walipomlilia BWANA katika shida yao, naye akawaokoa kutoka taabu yao. Akalituma neno lake na kuwaponya, akawaokoa kutoka maangamizo yao. Basi na wamshukuru BWANA kwa upendo wake usiokoma, na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu. Na watoe dhabihu za kushukuru, na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.