Zaburi 103:6-22
Zaburi 103:6-22 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Mwenyezi Mungu hutenda haki, naye huwapa hukumu ya haki wote wanaodhulumiwa. Alimjulisha Musa njia zake, na watu wa Israeli matendo yake. Mwenyezi Mungu ni mwingi wa huruma na mwenye neema; si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo. Yeye hatalaumu siku zote, wala haweki hasira yake milele, yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu. Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia, ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha; kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi. Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake, ndivyo Mwenyezi Mungu anavyowahurumia wale wanaomcha; kwa kuwa anajua tulivyoumbwa, anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi. Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani, anachanua kama ua la kondeni; upepo huvuma juu yake nalo hutoweka, mahali pake hapalikumbuki tena. Lakini kutoka milele hata milele upendo wa Mwenyezi Mungu uko kwa wale wamchao, nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao: kwa wale walishikao agano lake na kukumbuka kuyatii mausia yake. Mwenyezi Mungu ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni, na ufalme wake unatawala vitu vyote. Mhimidini Mwenyezi Mungu, enyi malaika wake, ninyi mlio mashujaa, mnaozitii amri zake, ninyi mnaotii neno lake. Mhimidini Mwenyezi Mungu, ninyi jeshi lake lote la mbinguni, ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake. Mhimidini Mwenyezi Mungu, enyi kazi zake zote kila mahali katika milki yake.
Zaburi 103:6-22 Biblia Habari Njema (BHN)
Mwenyezi-Mungu huhukumu kwa haki; huwajalia wanaodhulumiwa haki zao. Alimjulisha Mose mwongozo wake, aliwaonesha watu wa Israeli matendo yake. Mwenyezi-Mungu ni mwenye rehema na huruma; ni mvumilivu na mwingi wa fadhili. Hatukemeikemei daima, wala hasira yake haidumu milele. Yeye hatuadhibu kama tunavyostahili; hatulipizi kadiri ya uovu wetu. Kama vile anga lilivyo juu mbali na dunia, ndivyo ulivyo mwingi wema wake kwa watu wanaomcha. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo azitengavyo dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba amhurumiavyo mwanawe, ndivyo Mwenyezi-Mungu awahurumiavyo wote wamchao. Mungu ajua mfumo wa nafsi zetu; ajua kwamba sisi ni mavumbi. Walakini binadamu, maisha yake ni kama nyasi tu; huchanua kama ua shambani: Upepo huvuma juu yake nalo latoweka; na mahali lilipokuwa hapaonekani tena. Lakini fadhili za Mwenyezi-Mungu hudumu milele, kwa wale wote wanaomheshimu; na wema wake wadumu vizazi vyote, kwa wote wanaozingatia agano lake, wanaokumbuka kutii amri zake. Mwenyezi-Mungu ameweka kiti chake cha enzi mbinguni; yeye anatawala juu ya vitu vyote. Enyi malaika wakuu, msifuni Mwenyezi-Mungu; mnaotimiza amri zake na kutekeleza neno lake! Enyi jeshi lote la mbinguni, msifuni Mwenyezi-Mungu; enyi watumishi wake mnaotekeleza matakwa yake! Msifuni Mwenyezi-Mungu enyi viumbe vyake vyote; msifuni popote mlipo katika milki yake. Ee nafsi yangu, umsifu Mwenyezi-Mungu!
Zaburi 103:6-22 Swahili Revised Union Version (SRUV)
BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa. Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake. BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatashutumu daima, Wala hatashika hasira yake milele. Hakututenda kulingana na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. Maana, kama mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Ndivyo fadhili zake zilivyo kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo anavyostawi. Maana upepo hupita juu yake, na kutoweka! Lisionekane mahali lilipokuwa tena. Bali fadhili za BWANA ni kwa wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ni kwa vizazi vyote; Kwa wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye. BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote. Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake. Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake. Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.
Zaburi 103:6-22 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, Na hukumu kwa wote wanaoonewa. Alimjulisha Musa njia zake, Wana wa Israeli matendo yake. BWANA amejaa huruma na neema, Haoni hasira upesi, ni mwingi wa fadhili. Yeye hatateta sikuzote, Wala hatashika hasira yake milele. Hakututenda sawasawa na hatia zetu, Wala hakutulipa kwa kadiri ya maovu yetu. Maana mbingu zilivyoinuka juu ya nchi, Kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, Ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. Kama vile baba awahurumiavyo watoto wake, Ndivyo BWANA anavyowahurumia wamchao. Kwa maana Yeye anatujua umbo letu, Na kukumbuka ya kuwa sisi tu mavumbi. Mwanadamu siku zake zi kama majani; Kama ua la kondeni ndivyo asitawivyo. Maana upepo hupita juu yake, kumbe haliko! Na mahali pake hapatalijua tena. Bali fadhili za BWANA zina wamchao Tangu milele hata milele, Na haki yake ina wana wa wana; Maana, wale walishikao agano lake, Na kuyakumbuka maagizo yake ili wayafanye. BWANA ameweka kiti chake cha enzi mbinguni, Na ufalme wake unavitawala vitu vyote. Mhimidini BWANA, enyi malaika zake, Ninyi mlio hodari, mtendao neno lake, Mkiisikiliza sauti ya neno lake. Mhimidini BWANA, enyi majeshi yake yote, Ninyi watumishi wake mfanyao mapenzi yake. Mhimidini BWANA, enyi matendo yake yote, Mahali pote pa milki yake. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA.