Methali 4:22-24
Methali 4:22-24 Biblia Habari Njema (BHN)
Maana hayo ni uhai kwa mtu anayeyapata, ni dawa kwa mwili wake wote. Linda moyo wako kwa uangalifu wote, maana humo zatoka chemchemi za uhai. Tenga mbali nawe lugha potovu; wala midomo yako isitamke maneno madanganyifu.
Methali 4:22-24 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote. Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Jiepushe na kinywa cha ujeuri, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
Methali 4:22-24 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Maana ni uhai kwa wale wazipatao, Na afya ya mwili wao wote. Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Kinywa cha ukaidi ukitenge nawe, Na midomo ya upotovu uiweke mbali nawe.
Methali 4:22-24 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata na afya kwa mwili wote wa mwanadamu. Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo, maana ndiko zitokako chemchemi za uzima. Epusha kinywa chako na ukaidi; weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako.