Methali 31:25-31
Methali 31:25-31 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema iko katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.
Methali 31:25-31 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Amevikwa nguvu na heshima, anaweza kucheka bila kuwa na hofu kwa siku zijazo. Huzungumza kwa hekima na mafundisho ya kuaminika yapo ulimini mwake. Huangalia mambo ya nyumbani mwake wala hali chakula cha uvivu. Watoto wake huamka na kumwita aliyebarikiwa, mumewe pia humsifu, akisema: “Wanawake wengi hufanya vitu vyenye sifa nzuri, lakini wewe umewapita wote.” Kujipamba ili kuvutia ni udanganyifu na uzuri unapita upesi, bali mwanamke anayemcha BWANA atasifiwa. Mpe thawabu anayostahili, nazo kazi zake na zimletee sifa kwenye lango la mji.
Methali 31:25-31 Biblia Habari Njema (BHN)
Nguvu na heshima ndizo sifa zake, hucheka afikiriapo wakati ujao. Hufungua kinywa kunena kwa hekima, huwashauri wengine kwa wema. Huchunguza yote yanayofanyika nyumbani mwake, kamwe hakai bure hata kidogo. Watoto wake huamka na kumshukuru, mumewe huimba sifa zake. Husema, “Wanawake wengi wametenda mambo ya ajabu, lakini wewe umewashinda wote.” Madaha huhadaa na uzuri haufai, bali mwanamke amchaye Mwenyezi-Mungu atasifiwa. Jasho lake lastahili kulipwa, shughuli zake hazina budi kuheshimiwa popote.
Methali 31:25-31 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Nguvu na hadhi ndiyo mavazi yake; Anaucheka wakati ujao. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema i katika ulimi wake. Huangalia sana njia za watu wa nyumbani mwake; Wala hali chakula cha uvivu. Wanawe huondoka na kumwita heri; Mumewe naye humsifu, na kusema, Binti za watu wengi wamefanya mema, Lakini wewe umewapita wote. Upendeleo hudanganya, na uzuri ni ubatili; Bali mwanamke amchaye BWANA, ndiye atakayesifiwa. Mpe mapato ya mikono yake, Na matendo yake yamsifu malangoni.