Methali 3:27-35
Methali 3:27-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Usimnyime mtu anayehitaji msaada, ikiwa unao uwezo wa kufanya hivyo. Usimwambie jirani yako aende zake hadi kesho, hali wewe waweza kumpa anachohitaji leo. Usipange maovu dhidi ya jirani yako, anayeishi karibu nawe bila wasiwasi. Usigombane na mtu bila sababu ikiwa hajakudhuru kwa lolote. Usimwonee wivu mtu mkatili, wala usiige mwenendo wake. Maana waovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; lakini yeye huwafanya marafiki zake wale walio wanyofu. Mwenyezi-Mungu huapiza nyumba za waovu, lakini huyabariki makao ya waadilifu. Yeye huwadharau wenye dharau, lakini huwafadhili wanyenyekevu. Wenye hekima watavuna heshima, lakini wapumbavu watapata fedheha.
Methali 3:27-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama. Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lolote. Usimhusudu mtu mwenye ujeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake. Maana mtu mjeuri ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki. Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.
Methali 3:27-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Usiwanyime watu mema yaliyo haki yao, Ikiwa katika uwezo wa mkono wako kuyatenda. Usimwambie jirani yako, Nenda, urudi halafu, na kesho nitakupa; Nawe unacho kitu kile karibu nawe. Usiwaze mabaya juu ya jirani yako, Ambaye anakaa karibu nawe na kujiona salama. Usishindane na mtu bila sababu, Ikiwa hakukudhuru kwa lo lote. Usimhusudu mtu mwenye jeuri, Wala usiichague mojawapo ya njia zake. Maana mtu mkaidi ni chukizo kwa BWANA, Bali siri yake ni pamoja na wanyofu. Laana ya BWANA i katika nyumba ya waovu, Bali huibariki maskani ya mwenye haki. Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema. Wenye hekima wataurithi utukufu, Bali kukuzwa kwa wapumbavu ni fedheha.
Methali 3:27-35 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Usizuie wema kwa wale wanaostahili ikiwa katika uwezo wako kutenda. Usimwambie jirani yako, “Njoo baadaye, nitakupa kesho”: wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe. Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako, ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini. Usimshtaki mtu bila sababu, wakati hajakutenda dhara lolote. Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri wala kuchagua njia yake iwayo yote, kwa kuwa BWANA humchukia mtu mpotovu, lakini siri yake iko kwa mwenye haki. Laana ya BWANA i juu ya nyumba ya mwovu, lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki. Huwadhihaki wale wanaodhihaki, lakini huwapa neema wale wanyenyekevu. Wenye hekima hurithi heshima, bali huwaaibisha wapumbavu.