Methali 26:1-28
Methali 26:1-28 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kama theluji wakati wa kiangazi au mvua wakati wa mavuno, ndivyo asivyostahili heshima mpumbavu. Kama shomoro apigapigavyo mabawa yake au mbayuwayu katika kuruka kwake kasi, ndivyo ilivyo laana isiyo na sababu haimpati mtu. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, nayo fimbo kwa migongo ya wapumbavu! Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama wewe mwenyewe utakuwa kama yeye. Mjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake, ama atakuwa mwenye hekima machoni pake mwenyewe. Kama vile ilivyo kujikata miguu au kunywa hasara, ndivyo ilivyo kutuma ujumbe kwa mkono wa mpumbavu. Kama miguu ya kiwete inavyoningʼinia ndivyo ilivyo mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama kufunga jiwe kwenye kombeo, ndivyo ilivyo kumpa mpumbavu heshima. Kama mwiba kwenye mkono wa mlevi ndivyo ilivyo mithali kinywani mwa mpumbavu. Kama mpiga upinde ambaye hujeruhi ovyo, ndivyo alivyo yeye aajiriye mpumbavu au yeyote apitaye njiani. Kama mbwa ayarudiavyo matapiko yake, ndivyo mpumbavu arudiavyo upumbavu wake. Je, unamwona mtu ajionaye mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Liko tumaini zaidi kwa mpumbavu kuliko kwake. Mvivu husema, “Yuko simba barabarani, simba mkali anazunguka mitaa!” Kama vile mlango ugeukavyo kwenye bawaba zake, ndivyo mvivu ajigeuzavyo kitandani mwake. Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani, naye huchoka kuupeleka kwenye kinywa chake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake mwenyewe, kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara. Kama yeye amkamataye mbwa kwa masikio, ndivyo alivyo mtu apitaye njiani na kujiingiza kwenye ugomvi usiomhusu. Kama mtu mwendawazimu atupaye vijinga vya moto au mishale ya kufisha, ndivyo alivyo mtu amdanganyaye jirani yake na kusema, “Nilikuwa nikifanya mzaha tu!” Bila kuni moto huzimika; pasipo uchongezi ugomvi humalizika. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, na kama kuni kwenye moto, ndivyo alivyo mtu mgomvi kwa kuchochea ugomvi. Maneno ya mchongezi ni kama chakula kitamu; huingia sehemu za ndani sana za mtu. Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya. Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake, lakini moyoni mwake huficha udanganyifu. Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu, lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko. Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake, kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia. Ulimi wa uongo, huwachukia wale unaowaumiza, nacho kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.
Methali 26:1-28 Biblia Habari Njema (BHN)
Heshima apewayo mpumbavu haimfai; ni kama theluji ya kiangazi, au mvua ya wakati wa mavuno. Kama shomoro au mbayuwayu wasiotua, kadhalika laana asiyostahili mtu haimtui. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu. Usimjibu mpumbavu kipumbavu, usije ukafanana naye. Mjibu mpumbavu kama ustahilivyo upumbavu wake, asije akajiona kuwa mwenye hekima zaidi. Kumtuma mpumbavu ujumbe, ni kama kujikata miguu au kujitafutia shida. Methali mdomoni mwa mpumbavu, ni kama miguu ya kiwete inayoninginia. Kumpa mpumbavu heshima, ni kama kufunga jiwe kwenye kombeo. Mpumbavu anayejaribu kutumia methali, ni kama mlevi anayejaribu kungoa mwiba mkononi. Mtu amwajiriye mpumbavu au mlevi, ni kama mpiga upinde anayejeruhi kila mtu. Mpumbavu anayerudiarudia upumbavu wake, ni kama mbwa anayekula matapishi yake. Wamwona mtu ajionaye kuwa mwenye hekima? Nakuambia mpumbavu ni nafuu kuliko huyo. Mvivu husema: “Huko nje kuna simba; siwezi kwenda huko.” Kama vile mlango uzungukiapo bawaba zake, ndivyo mvivu juu ya kitanda chake. Mvivu huutia mkono wake katika sahani ya chakula, lakini hawezi kuuinua hadi mdomoni. Mvivu hujiona kuwa mwenye hekima kuliko watu saba wawezao kujibu kwa busara. Ajiingizaye katika ugomvi usiomhusu, ni kama mtu amshikaye masikio mbwa anayepita. Kama mwendawazimu achezeavyo mienge, au mishale ya kifo, ndivyo alivyo mtu ampotoshaye jirani, kisha aseme, “Nilikuwa natania tu!” Bila kuni, moto huzimika; bila mchochezi, ugomvi humalizika. Kama vile makaa au kuni huchochea moto, ndivyo mgomvi achocheavyo ugomvi. Maneno ya msengenyaji ni kama kitoweo; hushuka mpaka ndani kabisa tumboni. Kama rangi angavu iliyopakwa kigae, ndivyo yalivyo maneno matamu yenye nia mbaya. Mwenye chuki huficha chuki yake kwa maneno mazuri, lakini huwa ana hila moyoni mwake. Akiongea vizuri usimwamini, moyoni mwake mna chuki chungu nzima. Huenda akaficha chuki yake, lakini nia zake mbaya zitajulikana kwa wote. Amchimbiaye mwenzake shimo, hutumbukia mwenyewe; abingirishaye jiwe litamrudia mwenyewe. Asemaye uongo huwachukia hao anaowaumiza, naye abembelezaye huleta maangamizi.
Methali 26:1-28 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu. Kama shomoro katika kutangatanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpati mtu. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye. Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake. Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao. Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye. Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake. Mtu mvivu hutia mkono wake katika sahani; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu. Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti; Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu? Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo. Nayo hushukia pande za ndani za tumbo. Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha. Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Ingawa chuki hufunikwa na hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia. Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.
Methali 26:1-28 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kama theluji wakati wa joto, na mvua wakati wa mavuno; Kadhalika heshima haimpasi mpumbavu. Kama shomoro katika kutanga-tanga kwake, Na kama mbayuwayu katika kuruka kwake; Kadhalika laana isiyo na sababu haimpigi mtu. Mjeledi kwa farasi, lijamu kwa punda, Na fimbo kwa mgongo wa mpumbavu. Usimjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Usije ukafanana naye. Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake. Apelekaye ujumbe kwa mkono wa mpumbavu Hujikata miguu, na kunywa hasara. Miguu yake achechemeaye huwa dhaifu; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Kama mfuko wa vito katika chungu ya mawe; Kadhalika mtu amheshimuye mpumbavu. Kama mwiba uingiao katika mkono wa mlevi; Kadhalika mithali katika kinywa cha mpumbavu. Fundi stadi hufanyiza vitu vyote; Bali amwajiriye mpumbavu ni kama awaajiriye watu wapitao. Kama vile mbwa arudiavyo matapiko yake; Kadhalika mpumbavu afanya upumbavu tena. Je! Wamwona mtu mwenye hekima machoni pake mwenyewe? Afadhali kumtumaini mpumbavu kuliko yeye. Mtu mvivu husema, Simba yuko njiani, Simba yuko katika njia kuu. Kama vile mlango ugeukavyo katika bawaba zake; Kadhalika mtu mvivu katika kitanda chake. Mtu mvivu hutia mkono wake sahanini; Kwamchosha kuupeleka tena kinywani pake. Mtu mvivu ni mwenye hekima machoni pake, Kuliko watu saba wawezao kutoa sababu. Mtu apitaye na kujisumbua kwa ugomvi usio wake; Ni kama mtu ashikaye mbwa kwa masikio yake. Kama mtu mwenye wazimu atupaye mienge, Na mishale, na mauti; Ndivyo alivyo amdanganyaye mwenzake, Na kusema, Je! Sikufanya mzaha tu? Moto hufa kwa kukosa kuni; Na bila mchongezi fitina hukoma. Kama makaa juu ya makaa yanayowaka, Na kama kuni juu ya moto; Ndivyo mtu mgomvi achocheavyo uadui. Maneno ya mchongezi ni kama vitoweo. Nayo hushukia pande za ndani za tumbo. Midomo ijipendekezayo pamoja na moyo mbaya Ni kama kigae kilichofunikizwa taka za fedha. Achukiaye huficha chuki kwa midomo yake; Naye huweka akiba ya hila moyoni mwake. Anenapo maneno mazuri usimsadiki; Kwa maana ana machukizo saba moyoni mwake. Ingawa chuki hufunikizwa kwa hila; Uovu wake utadhihirika mbele ya kusanyiko. Achimbaye shimo atatumbukia mwenyewe; Naye abingirishaye jiwe litamrudia. Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi; Na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu.