Methali 25:1-7
Methali 25:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Hizi nazo ni methali nyingine za mfalme Solomoni walizonakili watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda. Mungu hutukuzwa kwa kuficha mambo, lakini mfalme hutukuzwa kwa yale anayoeleza. Kama zilivyo mbali mbingu na kirefu kina cha ardhi ndivyo zisivyochunguzika akili za mfalme. Toa takataka katika fedha, na mhunzi atakutengenezea chombo kizuri. Waondoe waovu mbele ya mfalme, na utawala wake utaimarika katika haki. Usijipendekeze kwa mfalme, wala usijifanye mtu mkubwa, maana ni heri kuambiwa, “Njoo huku mbele”, kuliko kuporomoshwa mbele ya mkuu. Mambo uliyoyaona kwa macho yako
Methali 25:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili. Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo. Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki. Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu; Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho
Methali 25:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Hizi nazo ni mithali za Sulemani, ambazo watu wa Hezekia, mfalme wa Yuda, walizinakili. Ni utukufu wa Mungu kuficha jambo; Bali ni utukufu wa mfalme kuchunguza jambo. Mbingu huenda juu sana, na nchi huenda chini; Lakini mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka katika fedha, Na chombo kitatokea kwa mtakasaji; Mwondoe asiye haki mbele ya mfalme, Na kiti chake cha enzi kitathibitika katika haki. Usijitukuze mbele ya uso wa mfalme; Wala usisimame mahali pa watu wakuu; Kwa maana ni heri kuambiwa, Njoo huku mbele; Kuliko kuwekwa nyuma machoni pa mkuu. Yale uliyoyaona kwa macho
Methali 25:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hizi ni mithali zaidi za Solomoni, zilizonakiliwa na watu wa Hezekia mfalme wa Yuda: Ni Utukufu wa Mungu kuficha jambo, bali ni utukufu wa wafalme kuchunguza jambo. Kama mbingu zilivyo juu na nchi ilivyo chini, ndivyo ambavyo mioyo ya wafalme haichunguziki. Ondoa takataka kwenye madini ya fedha, nako ndani yake kutatokea chombo cha mfua fedha. Ondoa waovu mbele ya mfalme, nacho kiti chake cha enzi kitaimarishwa kwa njia ya haki. Usijikweze mwenyewe mbele ya mfalme, wala usidai nafasi miongoni mwa watu wakuu; ni afadhali yeye akuambie, “Njoo huku juu,” kuliko yeye kukuaibisha mbele ya mkuu.