Methali 23:17-35
Methali 23:17-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa; Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika. Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema. Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu. Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee. Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu. Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia. Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa. Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni mtego wa shimo jembamba. Naam, huotea kama mnyang'anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu. Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiutazame mvinyo iwapo ni mwekundu; uitiapo bilauri rangi yake, ushukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Methali 23:17-35 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Usiuruhusu moyo wako kuwaonea wivu wenye dhambi, bali kila mara uwe na bidii katika kumcha Mwenyezi Mungu. Hakika kuna tumaini la baadaye kwa ajili yako, nalo tarajio lako halitakatiliwa mbali. Sikiliza, mwanangu na uwe na hekima, weka moyo wako kwenye njia iliyo sawa. Usiwe miongoni mwa wanywao mvinyo, au wale walao nyama kwa pupa, kwa maana walevi na walafi huwa maskini, nako kusinzia huwavika matambara. Msikilize baba yako, aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako atakapokuwa mzee. Nunua kweli wala usiiuze, pata hekima, adabu na ufahamu. Baba wa mwenye haki ana furaha kubwa, naye aliye na mwana mwenye hekima humfurahia. Baba yako na mama yako na wafurahi, mama aliyekuzaa na ashangilie! Mwanangu, nipe moyo wako, macho yako na yafuate njia zangu, kwa maana kahaba ni shimo refu na mwanamke mpotovu ni kisima chembamba. Kama mnyang’anyi, hungojea akivizia, naye huzidisha wasio waaminifu miongoni mwa wanaume. Ni nani mwenye ole? Ni nani mwenye huzuni? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye malalamiko? Ni nani aliye na majeraha yasiyo na sababu? Ni nani mwenye macho mekundu? Ni hao wanaokaa sana kwenye mvinyo, hao wanaoenda kuonja mabakuli ya mvinyo uliochanganywa. Usiukodolee macho mvinyo ukiwa mwekundu, unapometameta kwenye bilauri, unaposhuka taratibu! Mwishowe huuma kama nyoka na kutia sumu yake kama nyoka mwenye sumu. Macho yako yataona mambo mageni, na moyo wako kuwazia mambo yaliyopotoka. Utakuwa kama alalaye baharini, alalaye juu ya kamba ya merikebu. Utasema, “Wamenipiga lakini sikuumia! Wamenichapa, lakini sisikii! Nitaamka lini ili nikanywe tena?”
Methali 23:17-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Moyo wako usiwahusudu wenye dhambi; Bali mche BWANA mchana kutwa; Maana bila shaka iko thawabu; Na tumaini lako halitabatilika. Sikia, mwanangu, uwe na hekima, Na kuuongoza moyo wako katika njia njema. Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu. Msikilize baba yako aliyekuzaa, Wala usimdharau mama yako akiwa mzee. Inunue kweli, wala usiiuze; Naam, hekima, na mafundisho, na ufahamu. Baba yake mwenye haki atashangilia; Naye amzaaye mtoto mwenye hekima atamfurahia. Na wafurahi baba yako na mama yako; Na afurahi aliyekuzaa. Mwanangu, nipe moyo wako; Macho yako yapendezwe na njia zangu. Kwa maana kahaba ni shimo refu; Na malaya ni rima jembamba. Naam, huotea kama mnyang’anyi; Huwaongeza wenye hila katika wanadamu. Ni nani apigaye, Yowe? Ni nani aliaye, Ole? Ni nani mwenye ugomvi? Ni nani mwenye mguno? Ni nani aliye na jeraha zisizo na sababu? Ni nani aliye na macho mekundu? Ni wale wakaao sana kwenye mvinyo; Waendao kutafuta divai iliyochanganyika. Usiitazame mvinyo iwapo ni nyekundu; Iitiapo bilauri rangi yake, ishukapo taratibu; Mwisho wake huuma kama nyoka; Huchoma kama fira. Macho yako yataona mambo mageni; Na moyo wako utatoa yaliyopotoka. Naam, utakuwa kama alalaye katikati ya bahari; Au kama yeye asinziaye juu ya mlingoti. Utasema, Wamenichapa wala sikuumia; Wamenipiga wala sina habari; Nitaamka lini, nitazidi kuitafuta tena.
Methali 23:17-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Moyo wako usiwaonee wivu wenye dhambi, ila endelea kumcha Mwenyezi-Mungu siku zote. Hakika kuna kesho ya milele, na tumaini lako halitakuwa bure. Sikia mwanangu, uwe na hekima; fikiria sana jinsi unavyoishi. Usiwe mmoja wa walevi wa divai, wala walafi wenye kupenda nyama, maana walevi na walafi wataishia kuwa maskini, anayetumia siku yake kusinzia atavaa matambara. Msikilize baba yako aliyekuzaa, wala usimdharau mama yako akizeeka. Nunua ukweli, wala usiuuze; nunua hekima, mafunzo na busara. Baba wa mtoto mwadilifu atajaa furaha; anayemzaa mtoto mwenye hekima atamfurahia. Wafurahishe baba na mama yako; mama aliyekuzaa na afurahi. Mwanangu, nisikilize kwa makini, shikilia mwenendo wa maisha yangu. Malaya ni shimo refu la kutega watu; mwanamke mgeni ni kama kisima chembamba. Yeye hunyemelea kama mnyanganyi, husababisha wanaume wengi kukosa uaminifu. Ni nani wapigao yowe? Ni nani wenye huzuni? Ni nani wenye ugomvi? Ni nani walalamikao? Ni nani wenye majeraha bila sababu? Ni nani wenye macho mekundu? Ni wale ambao hawabanduki penye divai, wale wakaao chonjo kuonja divai iliyokolezwa. Usiitamani divai hata kwa wekundu wake, hata kama inametameta katika bilauri, na kushuka taratibu unapoinywa. Mwishowe huuma kama nyoka; huchoma kama nyoka mwenye sumu. Macho yako yataona mauzauza, moyo wako utatoa mambo yaliyopotoka. Utakuwa kama mtu alalaye katikati ya bahari, kama mtu alalaye juu ya mlingoti wa meli. Utasema, “Walinichapa, lakini sikuumia; walinipiga, lakini sina habari. Nitaamka lini? Ngoja nitafute kinywaji kingine!”