Methali 23:1-8
Methali 23:1-8 Biblia Habari Njema (BHN)
Ukiketi kula pamoja na mtawala, usisahau hata kidogo uko pamoja na nani. Zuia sana hamu yako, ikiwa wewe wapenda sana kula. Usitamani vyakula vyake vizuri, maana vyaweza kukudanganya. Ikiwa unayo hekima ya kutosha, usijitaabishe kutafuta utajiri. Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafla, ukaruka na kutowekea angani kama tai. Usile chakula cha mtu bahili, wala usitamani mapochopocho yake, maana moyoni mwake anahesabu unachokula. Atakuambia, “Kula, kunywa!” Lakini moyoni mwake hayuko pamoja nawe. Utatapika vipande ulivyokula; shukrani zako zote zitakuwa za bure.
Methali 23:1-8 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Utakapoketi kwa chakula pamoja na mtawala, Mwangalie sana yeye aliye mbele yako. Tena ujitie kisu kooni, Kama ukiwa mlafi. Usivitamani vyakula vyake vya anasa; Kwa maana ni vyakula vya hila. Usijitaabishe ili kupata utajiri; Acha kuzitegemea akili zako mwenyewe. Je! Utavikazia macho vile ambavyo si kitu? Maana bila shaka mali hujifanyia mabawa, Kama tai arukaye mbinguni. Usile mkate wa mtu mwenye husuda; Wala usivitamani vyakula vyake vya anasa; Maana aonavyo nafsini mwake, ndivyo alivyo. Akuambia, Haya, kula, kunywa; Lakini moyo wake hauwi pamoja nawe. Tonge lile ulilokula utalitapika, Na maneno yako matamu yatakupotea.
Methali 23:1-8 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Uketipo kula chakula na mtawala, angalia vyema kile kilicho mbele yako, na utie kisu kooni mwako kama ukiwa mlafi. Usitamani vyakula vyake vitamu kwa kuwa chakula hicho ni cha hila. Usijitaabishe ili kuupata utajiri, uwe na hekima kuonyesha kujizuia. Kufumba na kufumbua utajiri hutoweka, huwa kama umepata mabawa ghafula, ukaruka na kutoweka angani kama tai. Usile chakula cha mtu mchoyo, usitamani vyakula vyake vitamu, kwa maana yeye ni aina ya mtu ambaye kila mara anafikiri juu ya gharama. Anakuambia, “Kula na kunywa,” lakini moyo wake hauko pamoja nawe. Utatapika kile kidogo ulichokula, nawe utakuwa umepoteza bure maneno yako ya kumsifu.
Methali 23:1-8 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)