Methali 22:17-21
Methali 22:17-21 Biblia Habari Njema (BHN)
Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima, elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu. Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni, na kuyakariri kila wakati. Ninayependa kumfundisha leo ni wewe, ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu. Nimekuandikia misemo thelathini, misemo ya maonyo na maarifa, ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli; na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi.
Methali 22:17-21 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli?
Methali 22:17-21 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Tega sikio lako uyasikie maneno ya wenye hekima, na kuuelekeza moyo wako kwa maarifa yangu; maana ni vizuri kuyahifadhi ndani yako, hali yakithibitika pamoja midomoni mwako. Ili matumaini yako uyaweke kwa BWANA, leo nimekujulisha wewe haya, naam, wewe. Je! Sikukuandikia mambo makuu juu ya mashauri na juu ya maarifa; ili kukujulisha hakika ya maneno ya kweli, uwarudishie wakutumao maneno ya kweli?
Methali 22:17-21 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Tega sikio na usikie misemo ya wenye hekima, elekeza moyo wako kwenye yale nifundishayo, kwa maana inapendeza unapoyahifadhi moyoni mwako na kuwa nayo yote tayari mdomoni mwako. Ili tumaini lako liwe katika Mwenyezi Mungu, hata wewe, ninakufundisha leo. Je, sijakuandikia misemo thelathini, misemo ya mashauri na maarifa, kukufundisha maneno ya kweli na ya kuaminika, ili uweze kutoa majibu sahihi kwake yeye aliyekutuma?