Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Methali 16:1-33

Methali 16:1-33 Biblia Habari Njema (BHN)

Binadamu hupanga mipango yake, lakini kauli ya mwisho ni yake Mwenyezi-Mungu. Matendo ya mtu huonekana kwake kuwa sawa, lakini Mwenyezi-Mungu hupima nia ya mtu. Mwekee Mwenyezi-Mungu kazi yako, nayo mipango yako itafanikiwa. Mwenyezi-Mungu ameumba kila kitu kwa kusudi lake; hata waovu kwa ajili ya siku ya maangamizi. Kila mwenye kiburi ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu; hakika mtu wa namna hiyo hataacha kuadhibiwa. Kwa utii na uaminifu mtu huondolewa dhambi, kwa kumcha Mwenyezi-Mungu huepuka uovu. Mwenyezi-Mungu akipendezwa na mwenendo wa mtu, huwageuza hata adui zake kuwa marafiki. Afadhali mali kidogo kwa uadilifu, kuliko mapato mengi kwa udhalimu. Mtu aweza kufanya mipango yake, lakini Mwenyezi-Mungu huongoza hatua zake. Mfalme huamua kwa maongozi ya Mungu; anapotoa hukumu hakosei. Mwenyezi-Mungu hutaka kipimo na mizani halali; mawe yote mfukoni ya kupimia ni kazi yake. Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu, maana msingi wa mamlaka yao ni haki. Mfalme hupendelea mtu asemaye kwa unyofu; humpenda mtu asemaye ukweli. Hasira ya mfalme ni kama mjumbe wa kifo; mtu mwenye busara ataituliza. Uso wa mfalme ukingaa kuna uhai; wema wake ni kama wingu la masika. Kupata hekima ni bora kuliko dhahabu; kupata akili ni chaguo bora kuliko fedha. Njia ya wanyofu huepukana na uovu; anayechunga njia yake huhifadhi maisha yake. Kiburi hutangulia maangamizi; majivuno hutangulia maanguko. Afadhali kuwa mnyenyekevu na kuwa maskini, kuliko kugawana nyara na wenye kiburi. Anayezingatia mafundisho atafanikiwa; heri mtu yule anayemtumainia Mwenyezi-Mungu. Mwenye hekima moyoni huitwa mwenye akili; neno la kupendeza huwavutia watu. Hekima ni chemchemi ya uhai kwake aliye nayo, bali upumbavu ni adhabu ya wapumbavu. Moyo wa mwenye hekima humwezesha kusema kwa busara; huyafanya maneno yake yawe ya kuvutia. Maneno mazuri ni kama asali; ni matamu rohoni na yenye kuupa mwili afya. Mtu aweza kuona njia yake kuwa sawa, lakini mwishowe humwongoza kwenye kifo. Hamu ya chakula humhimiza mfanyakazi, maana njaa yake humsukuma aendelee. Mtu mwovu hupanga uovu; maneno yake ni kama moto mkali. Mtu mpotovu hueneza ugomvi, mfitini hutenganisha marafiki. Mtu mkatili humshawishi jirani yake; humwongoza katika njia mbaya. Anayekonyeza jicho kwa hila amepanga maovu; anayekaza midomo amekwisha nuia mabaya. Kuwa na mvi za uzee ni taji la utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu. Asiye mwepesi wa hasira ni bora kuliko mwenye nguvu; aitawalaye nafsi yake ni bora kuliko autekaye mji. Kura hupigwa kujua yatakayotukia, lakini uamuzi ni wake Mwenyezi-Mungu.

Shirikisha
Soma Methali 16

Methali 16:1-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatakuwa kweli. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake. Kukata maneno huwa katika midomo ya mfalme; Kinywa chake hakitakosa katika hukumu. Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA; Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake. Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki. Midomo ya haki ni furaha ya wafalme; Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa. Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza. Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme, Na fadhili zake ni kama wingu la masika. Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha. Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake. Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi. Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri. Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu. Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao. Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake. Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Nafsi yake mfanyakazi hujifanyia kazi; Maana kinywa chake humtia bidii. Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara; Katika midomo yake mna moto uteketezao. Mtu mshupavu huleta fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki. Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema. Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya. Kichwa chenye mvi ni taji la utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki. Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji. Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Shirikisha
Soma Methali 16

Methali 16:1-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Maandalio ya moyo ni ya mwanadamu; Bali jawabu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu ni safi machoni pake mwenyewe; Bali BWANA huzipima roho za watu. Mkabidhi BWANA kazi zako, Na mawazo yako yatathibitika. BWANA amefanya kila kitu kwa kusudi lake; Naam, hata wabaya kwa siku ya ubaya. Kila mwenye moyo wa kiburi ni chukizo kwa BWANA; Hakika, hatakosa adhabu. Kwa rehema na kweli uovu husafishwa; Kwa kumcha BWANA watu hujiepusha na maovu. Njia za mtu zikimpendeza BWANA, Hata adui zake huwapatanisha naye. Afadhali mali kidogo pamoja na haki, Kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake; Bali BWANA huziongoza hatua zake. Kukata maneno huwa katika midomo ya mfalme; Kinywa chake hakitakosa katika hukumu. Mizani ya haki na vitanga vyake ni vya BWANA; Mawe yote ya mfukoni ni kazi yake. Wafalme wakitenda yasiyo haki ni chukizo; Maana kiti cha enzi huthibitika kwa haki. Midomo ya haki ni furaha ya wafalme; Nao humpenda yeye asemaye yaliyo sawa. Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza. Kuna uhai katika nuru ya uso wa mfalme, Na fadhili zake ni kama wingu la masika. Si afadhali kupata hekima kuliko dhahabu? Naam, yafaa kuchagua ufahamu kuliko fedha. Njia kuu ya mwenye haki ni kujitenga na uovu; Yeye ashikaye njia yake huihifadhi nafsi yake. Kiburi hutangulia uangamivu; Na roho yenye kutakabari hutangulia maanguko. Afadhali kuwa na roho ya unyenyekevu pamoja na maskini, Kuliko kugawanya nyara pamoja na wenye kiburi. Atakayelitafakari neno atapata mema; Na kila amwaminiye BWANA ana heri. Aliye na hekima moyoni ataitwa mwenye busara; Utamu wa maneno huongeza elimu. Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwake aliye nao; Bali kufundishwa kwa wapumbavu ni upuzi wao. Moyo wake mwenye hekima hufundisha kinywa chake; Huzidisha elimu ya midomo yake. Maneno yapendezayo ni kama sega la asali; Ni tamu nafsini, na afya mifupani. Iko njia ionekanayo kuwa sawa machoni pa mtu; Lakini mwisho wake ni njia za mauti. Nafsi yake mfanya kazi hujifanyia kazi; Maana kinywa chake humtia bidii. Mtu asiyefaa kitu huchimba shimo la madhara; Katika midomo yake mna moto uteketezao. Mtu mshupavu huondokesha fitina; Na mchongezi huwafarakanisha rafiki. Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema. Afumbaye macho, kusudi lake ni kuwaza yaliyopotoka; Aikazaye midomo yake hutokeza mabaya. Kichwa chenye mvi ni taji ya utukufu, Kama kikionekana katika njia ya haki. Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji. Kura hutupwa katika mikunjo ya nguo; Lakini hukumu zake zote ni za BWANA.

Shirikisha
Soma Methali 16

Methali 16:1-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)

Mipango ya moyoni ni ya mwanadamu, bali jibu la ulimi hutoka kwa BWANA. Njia zote za mtu huonekana safi machoni pake mwenyewe, bali makusudi hupimwa na BWANA. Mkabidhi BWANA lolote ufanyalo, nayo mipango yako itafanikiwa. BWANA hufanya kila kitu kwa kusudi lake mwenyewe; hata waovu kwa siku ya maangamizi. BWANA huwachukia sana wote wenye kiburi cha moyo. Uwe na hakika kwa hili: Hawataepuka kuadhibiwa. Kwa upendo na uaminifu uovu huondolewa; kwa kumcha BWANA mtu hujiepusha na ubaya. Njia za mtu zinapompendeza BWANA, huwafanya hata adui zake waishi naye kwa amani. Afadhali kitu kidogo pamoja na haki kuliko mapato mengi pamoja na udhalimu. Moyo wa mtu huifikiri njia yake, bali BWANA huelekeza hatua zake. Midomo ya mfalme huzungumza kwa hekima ya kiungu, wala kinywa chake hakipotoshi haki. Vipimo na mizani za halali hutoka kwa BWANA; mawe yote ya kupimia yaliyo katika mfuko ameyafanya yeye. Wafalme huchukia sana kutenda maovu, kwa maana kiti cha ufalme hufanywa imara kwa njia ya haki. Wafalme hufurahia midomo ya uaminifu; humthamini mtu asemaye kweli. Ghadhabu ya mfalme ni mjumbe wa mauti, bali mtu mwenye hekima ataituliza. Uso wa mfalme ungʼaapo, inamaanisha uhai; upendeleo wake ni kama wingu la mvua wakati wa vuli. Ni bora kiasi gani kupata hekima kuliko dhahabu, kuchagua ufahamu kuliko fedha! Njia kuu ya wanyofu huepuka ubaya; yeye aichungaye njia yake, huchunga maisha yake. Kiburi hutangulia maangamizi, roho ya majivuno hutangulia maanguko. Ni afadhali kuwa mnyenyekevu katika roho miongoni mwa walioonewa kuliko kugawana nyara pamoja na wenye kiburi. Yeyote anayekubali mafundisho hustawi, tena amebarikiwa yeye anayemtumaini BWANA. Wenye hekima moyoni huitwa wenye ufahamu, na maneno ya kupendeza huchochea mafundisho. Ufahamu ni chemchemi ya uzima kwa wale walio nao, bali upumbavu huleta adhabu kwa wapumbavu. Moyo wa mtu mwenye hekima huongoza kinywa chake, na midomo yake huchochea mafundisho. Maneno ya kupendeza ni kama sega la asali, ni matamu kwa nafsi na uponyaji kwenye mifupa. Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu, bali mwisho wake huelekeza mautini. Shauku ya mfanyakazi humhimiza kufanya kazi; njaa yake humsukuma aendelee. Mtu mbaya kabisa hupanga mabaya, maneno yake ni kama moto uunguzao. Mtu mpotovu huchochea ugomvi, nayo maongezi ya upuzi hutenganisha marafiki wa karibu. Mtu mkali humvuta jirani yake na kumwongoza katika mapito yale mabaya. Yeye akonyezaye kwa jicho lake anapanga upotovu; naye akazaye midomo yake amenuia mabaya. Mvi ni taji ya utukufu; hupatikana kwa maisha ya uadilifu. Ni afadhali mtu mstahimilivu kuliko shujaa, mtu anayeitawala hasira yake kuliko yule autekaye mji. Kura hupigwa kwa siri, lakini kila uamuzi wake hutoka kwa BWANA.

Shirikisha
Soma Methali 16