Methali 14:23-35
Methali 14:23-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. Taji ya wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu. Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya. Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu. Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake. Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika. Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote. Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Methali 14:23-35 Biblia Habari Njema (BHN)
Bidii katika kila kazi huleta faida, lakini maneno matupu huleta umaskini. Mali ni taji ya fahari ya wenye hekima, lakini ujinga ni shada la wapumbavu. Shahidi wa kweli huokoa maisha, lakini msema uongo ni msaliti. Amchaye Mwenyezi-Mungu ana tumaini imara, na watoto wake watapata kimbilio salama. Kumcha Mwenyezi-Mungu ni chemchemi ya uhai; humwezesha mtu kuepa mitego ya kifo. Fahari ya mfalme ni wingi wa watu wake, lakini bila watu mtawala huangamia. Mtu asiye mwepesi wa hasira ana busara kubwa, lakini akasirikaye upesi hukuza upumbavu. Amani rohoni humpa mtu afya, lakini tamaa huozesha mifupa. Anayemdhulumu maskini anamtukana Muumba wake, lakini amwoneaye huruma mhitaji anamtukuza Mungu. Mwovu huangamizwa kwa matendo yake maovu, lakini mwadilifu hupata usalama kwa unyofu wake. Hekima imo moyoni mwa mtu mwenye busara; haipatikani kamwe mioyoni mwa wapumbavu. Uadilifu hukuza taifa, lakini dhambi ni balaa kwa taifa lolote. Mfalme humfadhili mtumishi atendaye kwa hekima, lakini hasira yake huwakumba watendao yasiyofaa.

Methali 14:23-35 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. Taji la wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu. Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya. Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu. Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake. Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika. Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wowote. Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali hasira yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Methali 14:23-35 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Katika kila kazi mna faida; Bali maneno ya midomo huleta hasara tu. Taji ya wenye hekima ni mali zao; Bali upumbavu wa wajinga ni upumbavu tu. Shahidi wa kweli huponya nafsi za watu; Bali atoaye uongo hudanganya. Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio. Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti. Utukufu wa mfalme ni wingi wa watu wake; Bali uchache wa watu ni uharibifu wa mkuu wao. Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu. Moyo ulio mzima ni uhai wa mwili; Bali husuda ni ubovu wa mifupa. Amwoneaye maskini humsuta Muumba wake; Bali yeye awahurumiaye wahitaji humheshimu. Mtu mbaya husukumwa chini katika kutenda mabaya kwake; Bali mwenye haki ana matumaini katika kufa kwake. Hekima hukaa katika moyo wake mwenye ufahamu; Bali yaliyo ndani ya wapumbavu hudhihirika. Haki huinua taifa; Bali dhambi ni aibu ya watu wo wote. Upendeleo wa mfalme humwelekea mtumwa atendaye kwa busara; Bali ghadhabu yake itakuwa juu yake aletaye aibu.
Methali 14:23-35 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida, bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu. Utajiri wa wenye hekima ni taji lao, bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu. Shahidi wa kweli huokoa maisha, bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu. Yeye amchaye Mwenyezi Mungu ana ngome salama, na kwa watoto wake itakuwa kimbilio. Kumcha Mwenyezi Mungu ni chemchemi ya uzima, ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti. Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme, bali pasipo watu mkuu huangamia. Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi, bali anayekasirika haraka huonesha upumbavu. Moyo wenye amani huupa mwili uzima, bali wivu huozesha mifupa. Yeye anayemdhulumu maskini humdharau Muumba wao, bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu. Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu, bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio. Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu. Haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu kwa watu wote. Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima, bali ghadhabu yake humwangukia mtumishi mwenye kuaibisha.