Methali 1:7-9
Methali 1:7-9 Biblia Habari Njema (BHN)
Kumcha Mwenyezi-Mungu ni msingi wa maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyapuuze mafundisho ya mama yako; hayo yatakupamba kilemba kichwani pako, kama mkufu shingoni mwako.
Methali 1:7-9 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.
Methali 1:7-9 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako, Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.
Methali 1:7-9 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Kumcha BWANA ndicho chanzo cha maarifa, lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu. Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako, wala usiyaache mafundisho ya mama yako. Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako, na mkufu wa kuipamba shingo yako.