Hesabu 7:89
Hesabu 7:89 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mose alipoingia kwenye Hema la Kukutania kuzungumza na BWANA, alisikia sauti ikisema naye kutoka kati ya wale makerubi wawili waliokuwa juu ya kile kiti cha rehema, juu ya Sanduku la Ushuhuda. Mose akazungumza naye.
Hesabu 7:89 Biblia Habari Njema (BHN)
Wakati Mose alipoingia ndani ya hema la mkutano ili kuongea na Mwenyezi-Mungu, alisikia sauti kutoka upande wa juu wa kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya sanduku la agano, kutoka kati ya wale viumbe wawili wenye mabawa.
Hesabu 7:89 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Kisha, Musa alipoingia ndani ya hema ya kukutania ili kunena na Mungu ndipo alipoisikia Sauti ikinena naye kutoka hapo juu ya kiti cha rehema, kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, ikitoka kati ya yale makerubi mawili; naye akanena naye.
Hesabu 7:89 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)