Hesabu 18:26
Hesabu 18:26 Biblia Habari Njema (BHN)
“Tena utawaambia Walawi maagizo yafuatayo: Wakati mtakapopokea zaka ambayo Mwenyezi-Mungu amewapa kutoka kwa Waisraeli iwe urithi wenu, mtanitolea mimi Mwenyezi-Mungu sehemu moja ya kumi ya zaka hiyo.
Hesabu 18:26 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Sema na Walawi na uwaambie: ‘Mtakapopokea zaka kutoka kwa Waisraeli ambayo ninawapa kama urithi wenu kutoka kwao, ni lazima mtoe sehemu ya kumi ya hiyo zaka kama sadaka kwa BWANA, iwe zaka ya hiyo zaka.
Hesabu 18:26 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Tena utanena na Walawi, na kuwaambia, Hapo mtakapoitwaa zaka mkononi mwa wana wa Israeli niliyowapa ninyi kutoka kwao kuwa urithi wenu, ndipo mtakaposongeza sadaka ya kuinuliwa kwa BWANA katika hiyo, iwe zaka katika hiyo zaka.
Hesabu 18:26 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)