Nehemia 12:27
Nehemia 12:27 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Wakati wa kuwekwa wakfu ukuta wa Yerusalemu, Walawi walitafutwa kule walikokuwa wakiishi, nao wakaletwa Yerusalemu kuadhimisha kwa shangwe huko kuweka wakfu kwa nyimbo za shukrani na kwa uimbaji wakitumia matoazi, vinubi na zeze.
Nehemia 12:27 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha wakati wa kuweka wakfu ukuta wa Yerusalemu Walawi walitafutwa kila mahali walipokaa ili kuja Yerusalemu kusherehekea kwa furaha pamoja na shukrani na nyimbo, wakitumia matoazi, vinubi na zeze.
Nehemia 12:27 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, ili waweze kusherehekea kuweka wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi.
Nehemia 12:27 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Basi, walipouweka wakfu ukuta wa Yerusalemu wakawatafuta Walawi katika mahali pao pote, ili kuwaleta Yerusalemu, wapate kufanya wakfu pamoja na furaha, na kwa shukrani, na kwa kuimba, kwa matoazi, vinanda na vinubi.