Marko 1:42-44
Marko 1:42-44 Biblia Habari Njema (BHN)
Mara ukoma ukamwacha mtu huyo, akatakasika. Kisha Yesu akamwambia aende zake upesi na kumwambia, “Angalia usimwambie mtu yeyote jambo hili, ila nenda ukajioneshe kwa kuhani na ukatoe sadaka kwa ajili ya kutakasika kwako kama alivyoamuru Mose kuwathibitishia kwamba umepona.”
Marko 1:42-44 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika. Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara, akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila nenda zako ukajioneshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa ajili ya kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.
Marko 1:42-44 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na mara ukoma wake ukamtoka, akatakasika. Akamkataza kwa nguvu, akamwondoa mara, akamwambia, Angalia, usimwambie mtu neno lolote, ila enenda zako ukajionyeshe kwa kuhani, ukatoe alivyoamuru Musa kwa kutakasika kwako, iwe ushuhuda kwao.
Marko 1:42-44 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Mara ukoma ukamtoka, naye akatakasika. Baada ya Yesu kumwonya vikali, akamruhusu aende zake akimwambia, “Hakikisha humwambii mtu yeyote habari hizi, bali nenda ukajionyeshe kwa kuhani, na ukatoe sadaka alizoagiza Mose kwa utakaso wako, ili kuwa ushuhuda kwao.”