Mika 4:1-7
Mika 4:1-7 Biblia Habari Njema (BHN)
Utakuja wakati ambapo mlima wa nyumba ya Mwenyezi-Mungu utakuwa mkubwa kuliko milima yote. Naam, utakwezwa juu ya vilima vyote. Watu wengi watamiminika huko, mataifa mengi yataujia na kusema: “Twendeni juu kwenye mlima wa Mwenyezi-Mungu, twende katika nyumba ya Mungu wa Yakobo, ili atufundishe njia zake, nasi tufuate nyayo zake. Maana mwongozo utatoka huko Siyoni; neno la Mwenyezi-Mungu huko Yerusalemu.” Mungu atasuluhisha mizozo ya mataifa mengi, atakata mashauri ya mataifa makubwa ya mbali. Nayo yatafua mapanga yao kuwa majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kupogolea. Taifa halitapigana na taifa lingine, wala hayatafanya tena mazoezi ya vita. Kila mtu atakaa kwa amani chini ya mitini na mizabibu yake, bila kutishwa na mtu yeyote. Mwenyezi-Mungu wa majeshi, ametamka yeye mwenyewe. Mataifa mengine hufuata njia zao, kwa kuitegemea miungu yao, lakini sisi twafuata njia zetu kwa kumtegemea Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, milele na milele. Mwenyezi-Mungu asema, “Siku ile nitawakusanya walemavu, naam, nitawakusanya waliochukuliwa uhamishoni, watu wale ambao niliwaadhibu. Hao walemavu ndio watakaobaki hai; hao waliochukuliwa uhamishoni watakuwa taifa lenye nguvu. Nami Mwenyezi-Mungu nitawatawala mlimani Siyoni, tangu wakati huo na hata milele.”
Mika 4:1-7 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njooni, twende juu mlimani kwa BWANA, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA litatoka Yerusalemu. Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha BWANA wa majeshi kimesema hivi. Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la BWANA, Mungu wetu, milele na milele. Katika siku ile, asema BWANA, nitamkusanya yeye achechemeaye, nami nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye niliyemtesa. Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu, na BWANA atawamiliki katika mlima Sayuni tangu sasa na hata milele.
Mika 4:1-7 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini itakuwa katika siku za mwisho, ya kwamba mlima wa nyumba ya BWANA utawekwa imara juu ya milima, nao utainuliwa juu ya vilima; na watu wa mataifa watauendea makundi makundi. Na mataifa mengi watakwenda na kusema, Njoni, twende juu mlimani kwa BWANA, na nyumbani kwa Mungu wa Yakobo; naye atatufundisha njia zake, nasi tutakwenda katika mapito yake; kwa maana katika Sayuni itatoka sheria, na neno la BWANA litatoka Yerusalemu. Naye atafanya hukumu kati ya watu wa kabila nyingi, naye atawakemea mataifa wenye nguvu walio mbali; nao watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao iwe miundu; taifa halitainua upanga juu ya taifa lingine, wala hawatajifunza vita tena kamwe. Bali wataketi kila mtu chini ya mzabibu wake, na chini ya mtini wake; wala hapana mtu atakayewatia hofu; kwa kuwa kinywa cha BWANA wa majeshi kimesema hivi. Kwa maana mataifa yote watakwenda, kila moja kwa jina la mungu wake, na sisi tutakwenda kwa jina la BWANA, Mungu wetu, milele na milele. Katika siku ile, asema BWANA, nitamkusanya yeye achechemeaye, nami nitamrudisha yeye aliyefukuzwa, na yeye niliyemtesa. Nami nitamfanya yeye aliyechechemea kuwa mabaki, na yeye aliyetupwa mbali kuwa taifa lenye nguvu, na BWANA atawamiliki katika mlima Sayuni tangu sasa na hata milele.
Mika 4:1-7 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Katika siku za mwisho mlima wa Hekalu la BWANA utaimarishwa kama mlima mkuu miongoni mwa milima yote; utainuliwa juu ya vilima, na watu wa mataifa watamiminika humo. Mataifa mengi yatakuja na kusema, “Njooni, twendeni mlimani mwa BWANA, kwenye nyumba ya Mungu wa Yakobo. Atatufundisha njia zake, ili tuweze kuenenda katika mapito yake.” Sheria itatoka Sayuni, neno la BWANA litatoka Yerusalemu. Atahukumu kati ya mataifa mengi, na ataamua migogoro ya mataifa yenye nguvu na yaliyo mbali. Watafua panga zao ziwe majembe, na mikuki yao kuwa miundu ya kukata matawi. Taifa halitainua upanga dhidi ya taifa jingine, wala hawatajifunza vita tena. Kila mtu ataketi chini ya mzabibu wake na chini ya mtini wake, wala hakuna mtu atakayewaogopesha, kwa kuwa BWANA Mwenye Nguvu Zote amesema. Mataifa yote yanaweza kutembea katika jina la miungu yao; sisi tutatembea katika jina la BWANA Mungu wetu milele na milele. BWANA “Katika siku hiyo,” asema BWANA, “nitawakusanya walemavu; nitawakusanya walio uhamishoni na wale niliowahuzunisha. Nitawafanya walemavu kuwa mabaki, wale waliofukuzwa kuwa taifa lenye nguvu. BWANA atatawala juu yao katika Mlima Sayuni kuanzia siku hiyo na hata milele.