Mathayo 5:38-40
Mathayo 5:38-40 Biblia Habari Njema (BHN)
“Mmesikia kwamba ilisemwa: ‘Jicho kwa jicho, jino kwa jino.’ Lakini mimi nawaambieni, usimlipize kisasi mtu mbaya. Mtu akikupiga kofi shavu la kulia, mgeuzie pia la pili. Mtu akikupeleka mahakamani kutaka kukuchukulia shati lako, mwache achukue pia koti lako.
Mathayo 5:38-40 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia.
Mathayo 5:38-40 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kulichukua shati lako, mwachie na koti pia.
Mathayo 5:38-40 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
“Mmesikia kwamba ilinenwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini kama mtu akikupiga kwenye shavu la kuume, mgeuzie na la pili pia. Kama mtu akitaka kukushtaki na kuchukua joho lako, mwachie achukue na koti pia.