Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Malaki 1:6-14

Malaki 1:6-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa. Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi. Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; je! Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi. Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu. Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika Mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika Mataifa, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mnalitia unajisi, kwa kuwa mwasema, Meza ya BWANA imetiwa unajisi; na matunda yake, yaani, nyama yake, hudharauliwa. Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA. Lakini na alaaniwe mtu mwenye kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa.

Shirikisha
Soma Malaki 1

Malaki 1:6-14 Biblia Habari Njema (BHN)

Mwenyezi-Mungu wa majeshi anawaambia hivi nyinyi makuhani mnaolidharau jina lake: “Mtoto humheshimu mzazi wake, na mtumishi humheshimu bwana wake. Ikiwa mimi ndiye Baba yenu, mbona mwanivunjia heshima? Ikiwa mimi ni bwana wenu, mbona hamniheshimu? Nanyi mnauliza, ‘Sisi tumekudharauje?’ Mwanidharau kwa kunitolea madhabahuni pangu tambiko ya chakula najisi. Lakini nyinyi mnauliza, ‘Tumekitiaje najisi?’ Mnakitia najisi kwa kuidharau madhabahu yangu. Mnaponitolea tambiko ya mnyama kipofu, au kilema, au mgonjwa, je, huo si uovu? Je, mtawala atapendezwa au kukufanyia hisani ukimpa zawadi ya mnyama kama huyo?” Kwa hiyo sasa enyi makuhani, mwombeni Mungu ili atuhurumie. Ikiwa mnamtolea matoleo ya aina hiyo, je, kweli atakuwa radhi nanyi? Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema, “Laiti angepatikana mtu mmoja miongoni mwenu ambaye angefunga milango ya hekalu ili msiwashe moto usiokubalika kwenye madhabahu yangu! Sipendezwi nanyi na sitaikubali tambiko yoyote mnayonitolea. Watu wa mataifa kote duniani, toka mawio ya jua hadi machweo yake, wanalitukuza jina langu. Kila mahali wananifukizia ubani na kunitolea tambiko zinazokubalika; maana jina langu linatukuzwa miongoni mwao. Lakini nyinyi mnalibeza jina langu pale mnapoichafua madhabahu yangu, na chakula mnachotoa juu yake mnakidharau. Mnasema, ‘Mambo haya yametuchosha mno,’ na mnanidharau. Mnaniletea tambiko za wanyama mliowapata kwa unyang'anyi, au walio vilema au wagonjwa. Je, nipokee tambiko hizo mikononi mwenu? Mimi Mwenyezi-Mungu nauliza. Na alaaniwe mtu yeyote anidanganyaye, ambaye huahidi kwa kiapo kunitolea tambiko mnyama safi kutoka katika kundi lake, lakini hunitolea tambiko mnyama mwenye kilema. Tazama, mimi ni mfalme mkuu, na watu wa mataifa yote hunicha.”

Shirikisha
Soma Malaki 1

Malaki 1:6-14 Swahili Revised Union Version (SRUV)

Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa. Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee mtawala wako; Je, Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi. Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; Je, Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi. Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yoyote mikononi mwenu. Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika mataifa, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mnalitia unajisi, kwa kuwa mwasema, Meza ya BWANA imetiwa unajisi; na matunda yake, yaani, nyama yake, hudharauliwa. Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA. Lakini na alaaniwe mtu adanganyaye, ambaye katika kundi lake ana dume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika mataifa.

Shirikisha
Soma Malaki 1

Malaki 1:6-14 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)

Mwana humheshimu baba yake, na mtumishi humcha bwana wake; basi, kama mimi ni baba yenu, heshima yangu iko wapi? Na kama mimi ni bwana wenu, kicho changu ki wapi? BWANA wa majeshi awauliza ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau jina langu. Nanyi mwasema, Tumelidharau jina lako kwa jinsi gani? Mnatoa chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu Nanyi mwasema, Sisi tumekutia unajisi kwa jinsi gani? Kwa sababu mwasema, Meza ya BWANA ni kitu cha kudharauliwa. Tena mtoapo sadaka aliye kipofu, si vibaya? Na mtoapo sadaka walio vilema na wagonjwa, si vibaya? Haya! Mtolee liwali wako; je! Atakuwa radhi nawe? Au atakukubali nafsi yako? Asema BWANA wa majeshi. Na sasa, nawasihi, ombeni fadhili za Mungu, ili atupe neema; ikiwa jambo hili limetoka katika mikono yenu; je! Atawakubali nafsi zenu? Asema BWANA wa majeshi. Laiti angekuwapo kwenu mtu mmoja wa kuifunga milango; msije mkawasha moto bure madhabahuni pangu! Sina furaha kwenu, asema BWANA wa majeshi, wala sitakubali dhabihu yo yote mikononi mwenu. Kwa maana tokea maawio ya jua hata machweo yake jina langu ni kuu katika Mataifa; na katika kila mahali unatolewa uvumba na dhabihu safi kwa jina langu; maana jina langu ni kuu katika Mataifa, asema BWANA wa majeshi. Lakini ninyi mnalitia unajisi, kwa kuwa mwasema, Meza ya BWANA imetiwa unajisi; na matunda yake, yaani, nyama yake, hudharauliwa. Tena mwasema, Tazama, jambo hili linatuchokesha namna gani! Nanyi mmelidharau, asema BWANA wa majeshi; nanyi mmeleta kitu kilichopatikana kwa udhalimu, na kilema, na kilicho kigonjwa; ndivyo mnavyoleta sadaka; je! Niikubali hii mikononi mwenu? Asema BWANA. Lakini na alaaniwe mtu mwenye kudanganya, ambaye katika kundi lake ana mume, akaweka nadhiri, ila amtolea Bwana kitu kilicho na kilema; kwa maana mimi ni Mfalme mkuu, asema BWANA wa majeshi, na jina langu latisha katika Mataifa.

Shirikisha
Soma Malaki 1

Malaki 1:6-14 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)

“Mwana humheshimu baba yake, naye mtumishi humheshimu bwana wake. Kama mimi ni baba, iko wapi heshima ninayostahili? Kama mimi ni bwana, iko wapi heshima ninayostahili?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Ni ninyi, enyi makuhani, mnaolidharau Jina langu. “Lakini mnauliza, ‘Tumelidharau Jina lako kwa namna gani?’ “Mnatoa sadaka chakula kilichotiwa unajisi juu ya madhabahu yangu. “Lakini ninyi mnauliza, ‘Tumekutia unajisi kwa namna gani?’ “Kwa kusema kuwa meza ya Mwenyezi Mungu ni ya kudharauliwa. Mnapoleta dhabihu za wanyama walio vipofu, je, hilo si kosa? Mnapoleta dhabihu zilizo vilema au wanyama wagonjwa, je, hilo si kosa? Jaribuni kuvitoa kwa mtawala wenu! Je, angefurahishwa nanyi? Je, atawakubalia?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Basi mwombeni Mungu awe na neema kwetu. Je, kwa sadaka kama hizo kutoka mikononi mwenu, atawapokea?” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Laiti mmoja wenu angeifunga milango ya Hekalu, ili msije mkawasha moto usiokuwa na faida juu ya madhabahu yangu! Sina furaha nanyi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, “nami sitaikubali sadaka toka mikononi mwenu. Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa, kuanzia mawio ya jua hata machweo yake. Kila mahali uvumba na sadaka safi zitaletwa kwa Jina langu, kwa sababu Jina langu litakuwa kuu miongoni mwa mataifa,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Lakini mnalinajisi Jina langu kwa kusema kuhusu meza ya Bwana, ‘Imetiwa unajisi pamoja na chakula chake. Ni ya kudharauliwa.’ Nanyi mnasema, ‘Mzigo gani huu!’ Nanyi mnaidharau kwa kiburi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. “Mnapowaleta wanyama mliopokonya kwa nguvu, walio vilema au walio wagonjwa na kuwatoa kama dhabihu, je, niwakubali kutoka mikononi mwenu?” asema Mwenyezi Mungu. “Amelaaniwa yeye adanganyaye, aliye na mnyama wa kiume anayekubalika katika kundi lake na kuweka nadhiri ya kumtoa, lakini akatoa dhabihu ya mnyama aliye na dosari kwa Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa mimi ni Mfalme Mkuu, nalo Jina langu linapaswa kuogopwa miongoni mwa mataifa,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.

Shirikisha
Soma Malaki 1