Luka 5:15-16
Luka 5:15-16 Biblia Habari Njema (BHN)
Lakini habari za Yesu zilizidi kuenea kila mahali. Watu makundi mengi wakakusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Lakini yeye alikwenda zake mahali pasipo na watu, akawa anasali huko.
Luka 5:15-16 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao. Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.
Luka 5:15-16 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini habari zake zikazidi kuenea, wakakutanika makutano mengi wamsikilize na kuponywa magonjwa yao. Lakini yeye alikuwa akijiepua, akaenda mahali pasipokuwa na watu, akaomba.
Luka 5:15-16 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Lakini habari zake Yesu zikazidi sana kuenea kotekote kuliko wakati mwingine wowote. Makutano makubwa ya watu yalikuwa yakikusanyika ili kumsikiliza na kuponywa magonjwa yao. Lakini mara kwa mara Yesu alijitenga nao ili kwenda mahali pa faragha kuomba.