Luka 24:50-53
Luka 24:50-53 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kuu. Nao daima walikuwa ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.
Luka 24:50-53 Biblia Habari Njema (BHN)
Kisha akawaongoza nje ya mji hadi Bethania, akainua mikono yake juu, akawabariki. Alipokuwa anawabariki, akawaacha; akachukuliwa mbinguni. Wao wakamwabudu, kisha wakarudi Yerusalemu wakiwa na furaha kubwa: Wakakaa muda wote hekaluni wakimsifu Mungu.
Luka 24:50-53 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akawaongoza mpaka Bethania, akainua mikono yake akawabariki. Ikawa katika kuwabariki, alijitenga nao; akachukuliwa juu mbinguni. Wakamwabudu; kisha wakarudi Yerusalemu wenye furaha kuu. Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.
Luka 24:50-53 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Akiisha kuwaongoza mpaka kwenye viunga vya Bethania, akainua mikono yake juu na kuwabariki. Alipokuwa anawabariki, akawaacha, akachukuliwa mbinguni. Kisha wakamwabudu na kurudi Yerusalemu wakiwa wamejawa na furaha kuu. Nao wakadumu ndani ya Hekalu wakimtukuza Mungu. Amen.