Luka 20:45-47
Luka 20:45-47 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu aliwaambia wanafunzi wake mbele ya watu wote, “Jihadharini na waalimu wa sheria ambao hupenda kupitapita wamevalia kanzu. Hupenda kusalimiwa na watu kwa heshima masokoni, huketi mahali pa heshima katika masunagogi na kuchukua nafasi za heshima katika karamu. Huwadhulumu wajane huku wakisingizia kuwa wema kwa kusali sala ndefu. Hao watapata hukumu kali zaidi!”
Luka 20:45-47 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Na watu wote walipokuwa wakimsikiliza, aliwaambia wanafunzi wake, Jihadharini na waandishi, wapendao kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni. Wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu. Hao watapata hukumu iliyo kuu.
Luka 20:45-47 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Na watu wote walipokuwa wakimsikiliza, aliwaambia wanafunzi wake, Jilindeni na waandishi, wapendao kutembea wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa masokoni, na kuketi mbele katika masinagogi, na viti vya mbele karamuni. Wanakula nyumba za wajane, na kwa unafiki husali sala ndefu. Hao watapata hukumu iliyo kuu.
Luka 20:45-47 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Wakati watu wote walikuwa wanamsikiliza, Isa akawaambia wanafunzi wake, “Jihadharini na walimu wa Torati. Wao hupenda kutembea wakiwa wamevaa mavazi marefu, na kusalimiwa kwa heshima masokoni. Hupenda kukaa kwenye viti vya mbele katika masinagogi, na kukaa kwenye nafasi za heshima katika karamu. Wao hula nyumba za wajane, na ili waonekane kuwa wema, wanasali sala ndefu. Watu kama hawa watapata hukumu iliyo kuu sana.”