Luka 18:31-33
Luka 18:31-33 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Yesu akawachukua wale wanafunzi wake kumi na wawili kando na kuwaambia, “Tunapanda kwenda Yerusalemu, na kila kitu kilichoandikwa na manabii kumhusu Mwana wa Adamu kitatimizwa. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa watu wasiomjua Mungu, nao watamdhihaki, watamtukana na kumtemea mate, watampiga mijeledi na kumuua. Naye siku ya tatu atafufuka.”
Luka 18:31-33 Biblia Habari Njema (BHN)
Yesu aliwachukua kando wale kumi na wawili, akawaambia, “Sikilizeni! Tunakwenda Yerusalemu na huko kila kitu kilichoandikwa na manabii kuhusu Mwana wa Mtu kitakamilishwa. Kwa maana atakabidhiwa kwa watu wa mataifa nao watamtendea vibaya na kumtemea mate. Watampiga mijeledi na kumuua; lakini siku ya tatu atafufuka.”
Luka 18:31-33 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Akawachukua wale Kumi na Wawili, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii yatatimizwa. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.
Luka 18:31-33 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Akawachukua wale Thenashara, akawaambia, Tazameni, tunapanda kwenda Yerusalemu, na mambo yote yatatimizwa, Mwana wa Adamu aliyoandikiwa na manabii. Kwa kuwa atatiwa mikononi mwa Mataifa, atafanyiwa dhihaka; atatendwa jeuri, na kutemewa mate; nao watampiga mijeledi, kisha watamwua; na siku ya tatu atafufuka.