Luka 18:15-17
Luka 18:15-17 Biblia Habari Njema (BHN)
Watu walimletea Yesu watoto wadogo ili awawekee mikono yake. Wanafunzi walipowaona, wakawazuia kwa maneno makali. Lakini Yesu akawaita kwake akisema: “Waacheni hao watoto waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni kwa ajili ya watu kama hawa. Nawaambieni kweli, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hataingia katika ufalme huo.”
Luka 18:15-17 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Wakamletea na watoto wachanga ili awaguse; lakini wanafunzi walipoona waliwakemea. Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambia, Mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.
Luka 18:15-17 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Wakamletea na watoto wachanga ili awaguse; lakini wanafunzi walipoona waliwakemea. Bali Yesu akawaita waje kwake, akasema, Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa kuwa watu kama hao ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambia, Mtu ye yote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hauingii kamwe.
Luka 18:15-17 Neno: Maandiko Matakatifu 2024 (NENO)
Pia, watu walikuwa wakimletea Isa watoto wachanga ili awaguse. Wanafunzi wake walipoona hivyo, wakawakemea. Lakini Isa akawaita wale watoto waje kwake, akasema, “Waacheni watoto wadogo waje kwangu, wala msiwazuie, kwa maana ufalme wa Mungu ni wa wale walio kama hawa. Amin, nawaambia, mtu yeyote asiyeupokea ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”