Luka 12:2-3
Luka 12:2-3 Biblia Habari Njema (BHN)
Kila kilichofunikwa kitafunuliwa, kila kilichofichika kitafichuliwa. Kwa hiyo, kila mliyosema gizani, watu watayasikia katika mwanga, na kila mliyonongona faraghani milango imefungwa, yatatangazwa juu ya nyumba.
Luka 12:2-3 Swahili Revised Union Version (SRUV)
Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana. Basi, yoyote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatatangazwa juu ya dari.
Luka 12:2-3 Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia (SUV)
Lakini hakuna neno lililositirika ambalo halitafunuliwa, wala lililofichwa ambalo halitajulikana. Basi, yo yote mliyosema gizani yatasikiwa mwangani; na mliyonena sikioni mwa mtu katika vyumba vya ndani, yatahubiriwa juu ya dari.
Luka 12:2-3 Neno: Bibilia Takatifu (NEN)
Hakuna jambo lolote lililositirika ambalo halitafunuliwa, au lililofichwa ambalo halitajulikana. Kwa hiyo, lolote mlilosema gizani litasikiwa nuruni. Na kile mlichonongʼona masikioni mkiwa kwenye vyumba vya ndani, kitatangazwa juu ya paa.